Guardian Angel akumbuka alivyofukuzwa kanisa kwa kuoa mwanamke mzee

Guardian alizidi kufichua kwamba maisha yake yalichukua mkondo mpya baada ya kukutana na Mchungaji Ababu, ambaye sasa ni babake wa kiroho.

Muhtasari
  • Mwimbaji huyo aliendelea kusema kuwa masaibu hayo yalimfanya aape kwamba hatarudi tena kanisani.
Image: INSTAGRAM// GUARDIAN ANGEL

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Guardian Angel amefichua jinsi alivyoteswa kanisani kwa kuoa mwanamke mzee.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa rekodi yake mpya ya "7 Heaven Music" Angel alikiri kwamba unyanyasaji huo ulimfanya kuacha kanisa kwa muda.

“Nilienda kanisani kuimba mahali fulani na niliteswa katika Kanisa hilo. Nilipofika mchungaji aliniambia kuwa wazee wameniagiza nisiimbe wala nisikanyage madhabahuni. Wote walibishana na baada ya dakika 30 mchungaji akakubali kwamba niimbe. Nilipoanza mchungaji alikasirika tena na kutaka kuninyang’anya kipaza sauti lakini mkewe akamuita,” Angel alisema kwa sehemu.

"Nilipomaliza, mchungaji alichukua kipaza sauti na kamwe hakukiri kwamba ilikuwa imeimbwa tu. Hiyo ilinifanya nichukie kanisa,".

Mwimbaji huyo aliendelea kusema kuwa masaibu hayo yalimfanya aape kwamba hatarudi tena kanisani.

“Nilianza kujiuliza, Kwani Kuoa bibi yangu kutafanya mpaka I don’t deserve to sing for God in church.

“Nilienda nyumbani na mke wangu na kumwambia kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya mwisho kuingia kanisani. Nilisema sitaingia katika kanisa lolote. Mabo ya Kanisa na mimi it is done. Nilisema nitakuwa nikisali chumbani kwangu lakini mke wangu aliendelea kwenda kanisani kwake,” aliongeza.

Guardian alizidi kufichua kwamba maisha yake yalichukua mkondo mpya baada ya kukutana na Mchungaji Ababu, ambaye sasa ni babake wa kiroho.

Anasema Ababu alikubali kutembea naye licha ya mambo yote mabaya yaliyokuwa yakisemwa juu yake.