Mwanamke tajiri kutoka London atema nyongo kuvutiwa na penzi la Harmonize

“Kwa sababu yuko single, ninaweza nikamuoa akaenda kukaa London, akafanyie muziki wake London. Hapo vipi Harmonize?" alisema mwanamke huyo.

Muhtasari

• "Nataka ahamishe muziki wake kwenda London, anajua kutunga sana, ananikosha,” aliongeza.

• “Yule mtoto anajua kuimba jamani, haswa alipotoa huu wimbo wake wa Single Again."

Harmonize
Harmonize
Image: Instagram

Mwanamke mmoja wa Tanzania mwenye makao yake mjini Uingereza, London amejitokeza bayana kutangaza jinsi gani anavyovutiwa na msanii Harmonize na hata kuweka wazi kwamba itakuwa ni bahati kubwa kwake kukubaliwa na msanii huyo kimapenzi.

Katika mahojiano ambayo yalipakiwa na mkuza maudhui Carry Mastory kwenye Instagram yake, mwanamke huyo aliyeonekana kuwa mwenye mali licha ya umri kusonga kumliko Harmonize alisema kwamba msanii huyo ndiye mpenzi wa ndoto zake tangia aanze kumuona miaka michache iliyopita.

“Yule mtoto anajua kuimba jamani, haswa alipotoa huu wimbo wake wa Single Again. Japo sijawahi kutana na yeye ana kwa ana lakini ana sauti nzuri sana yule mtoto. Angekuwa London ningemchumbia, sisi London wanawake tunachumbia, sisi ndio tunafanya kuchumbia,” mwanamke huyo alisema.

“Kwa sababu yuko single, ninaweza nikamuoa akaenda kukaa London, akafanyie muziki wake London. Hapo vipi Harmonize? Unasikia, nataka kuupeleka London. Nataka ahamishe muziki wake kwenda London, anajua kutunga sana, ananikosha,” aliongeza.

Mei mwaka huu, miezi kadhaa baada ya kujivinjari na mwigizaji Fridah Kajala, Harmonize alidokeza kuwa kwenye uhusiano mpya na mwanamke mnene kutoka Rwanda anayefahamika kwa jina la Phiona aka Yolo Queen.

Alionyesha upendo wake kwa mwanamitindo huyo, akisema kwamba walikuwa wamefahamiana kwa miaka minne. Harmonize hata aliapa kupata tattoo yake ya mwisho ya uso wake.

"Ulipopata pesa na umaarufu ulimwengu ni mgumu sana. Ni ngumu sana kujua ni nani aliye halisi kwako. Nimekuwa nikizungumza na Phiona zaidi ya miaka 4. Nimekuwa karibu, yeye amekuwa karibu. Daima tunaanza mazungumzo tena. Ninahisi ni wakati wa kukuonyesha jinsi nilivyo mwanaume halisi. Nakupenda ndani kabisa. Wewe juu ya kila msichana niliyekutana naye maishani mwangu,” alisema kwenye simulizi zake za Insta.

Walakini tangu wakati huo hajawahi kushiriki sasisho kuhusu uhusiano wao.