Jacky Matubia akiri kutokuwa na kanisa, ingawa yeye huomba Mungu wake kila mara

Siendi Kanisa ila nina njia zangu za kumfikia Mungu wangu Muigizaji Matubia asema

Muhtasari

•Mwanadamu kwa maisha yake ana jinsi ambavyo hushirikisha  uhusiano  wa karibu na Mungu wake kwa njia tofauti hata mbila ya kuenda kanisa alisema

Jackie Matubia
Jackie Matubia
Image: instagram

Muigizaji maarufu wa Kenya Jackie Matubia amejibu wazi baada ya kutakiwa kubaini iwapo yeye huenda kanisani.

Jackie alifunguka na kusimulia kuwa kwa maisha yake hajapata kanisa lolote ambalo anaweza kushiriki.

"Bado sijapata kanisa .....bado sijapata najua marafiki wangu wengi wanashiriki makanisa mbali mbali ila kwangu bado sijafanikiwa kupata kanisa ambalo nawezakushiriki",alisema muigizaji huyo.

"Mwanadamu kwa maisha yake ana jinsi ambavyo hushirikisha  uhusiano  wa karibu na Mungu wake kwa njia tofauti hata bila ya kwenda kanisa,"alisema Jackie Matubia.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja Matubia alisimulia kuwa kukosa kwenda kanisa kwake ni sawa ila alidokeza kwamba yeye yuko na uhusiano mzuri na Mungu wake.

"Marafiki wangu kuenda kanisa   haimanishi kuwa mimi nafaa kufuata mfano wao kila mmoja kuna jinsi ambavyo hufikisha maombi yake kwa Mungu kwa maisha yangu niko baraka ya za Mungu,"alisema.

Muigizaji huyu alisema kuwa yeye anafurahia maisha yake na jinsi humtumikia Muumba wake bila kushiriki kwa kanisa lolote kwani kulingana naye makanisa ni mengi ila hajapata la kujiunga nalo.