Mashabiki wapagawa Raila akiwahutubia live kutoka kwa akaunti ya TikTok ya Nyako

Natumai tunaweza kutembea pamoja na kwa pamoja tutafanikiwa. Tutashinda. Aluta continua,” alisema Odinga.

Muhtasari

• "Huyu ni Baba anazungumza na nyinyi watu. Hamjambo?" Raila alianza hotuba yake.

Nyako na Raila
Nyako na Raila
Image: Maktaba

Maelfu ya wafuasi wa kinara wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga jioni ya Alhamisi walipata nafasi adimu ya kumsikiliza kinara huyo akiwahutubia kwa mara ya kwanza kupitia mtandao wa TikTok.

Odinga alitokea katika kipindi cha moja kwa moja kwenye TikTok ya Nyako na kuwazungumzia mashabiki wake ambao walionesha furaha ghaya.

Nyako alikutana na Raila katika eneo lililofanana na nyumbani kwake, naye akamgeukia kamera, jambo ambalo liliwaacha watu wengi waliokuwa kwenye video hiyo ya moja kwa moja wakishangilia sana.

"Huyu ni Baba anazungumza na nyinyi watu. Hamjambo? Nina hapa binti mmoja ambaye amekuja kutoka Ujerumani ambaye ananiambia kuwa yeye ni bingwa wa TikTok na kwamba nahitaji kuzungumza na watazamaji kwenye TikTok.”

“Ninapenda TikTok na ninawapenda ninyi watu. Nimefurahi sana kuwafanya marafiki. Natumai tunaweza kutembea pamoja na kwa pamoja tutafanikiwa. Tutashinda. Aluta continua,” alisema.

Baba alikuwa amevalia shati la bluu bahari; alizungumza na kamera na pia akaendelea kumwangalia Nyako aliyekuwa amesimama nyuma ya simu, mwanasiasa huyo mkongwe akipata raha na mashabiki wake kupitia video ya moja kwa moja ya shabiki mwingine.

Tazama video hii hapa,