Abel Mutua ni baba mwenye furaha baada ya bintiye kuhitimu

"Wa kwanza nyumbani kwetu kuvaa kofia ya kuhitimu. Mama yako hapa aligraduate na dress ya maternity. So proud baby!" Abel aliandika.

Muhtasari

•Baba wa mtoto mmoja alishindwa kujizuia kukumbusha jinsi mkewe alivyohitimu akiwa na ujauzito.

Binti wa Abel Mutua
Binti wa Abel Mutua
Image: Instagram

Abel Mutua ni baba mwenye fahari baada ya bintiye kufuzu.

Alikuwa miongoni mwa mamilioni ya Wakenya waliokuwa wakifanya mtihani wao wa KCPE.

Baba wa mtoto mmoja alishindwa kujizuia kukumbusha jinsi mkewe alivyohitimu akiwa na ujauzito.

"Aaaaand it's done!!!! So proud of you Mumbus. Wa kwanza nyumbani kwetu kuvaa kofia ya kuhitimu. Mama yako hapa aligraduate na dress ya maternity. So proud baby! ❤️❤️❤️'

Judy hakuweza kuficha furaha yake kwa bintiye kujiunga na kidato cha kwanza.

'Tumehitimu! Sasa ni rasmi, mono inaingia! '

Katika mahojiano yaliyopita Nyawira alifichua kuwa alirejea shuleni wiki mbili baada ya kujifungua

'Ilinibidi kurejea shuleni wiki mbili baada ya kujifungua.

Nilikuwa nikifanya kazi kwenye mradi wangu. Nilikuwa na chaguo la kuahirisha kwa mwaka mmoja lakini sikutaka.

Nilijiweka katika hali hiyo na ningeishughulikia."

Judy alimsifu Abel kwa kuwa baba wa sasa tangu siku ya kwanza.