"Sijaolewa kuja kuangaliana na bwana!" Nandy ajibu kuhusu kuwa na mimba ya pili

Nandy kwa kujibu alisema kwa utani kwamba kupata mimba ni sehemu ya kazi au tuseme jukumu kuu kwenye ndoa kwani hakuolewa ili kuja kukaa tu na kuangaliana na mume wake.

Muhtasari

• Nandy alikuwa amevalia kiguo kifupi na kwa hakika kitumbo kama kilionekana kutokea upande wa mbele hadi kuvutia idadi kubwa ya maswali hayo.

Nandy
Nandy
Image: Instagram

Baada ya mashabiki wengi kukisia kwamba msanii Nandy ana mimba ya pili, ikiwa ni mwaka mmoja tu baada ya kufnga harusi na kupata mtoto wa kwanza na mumewe, Billnass, msanii huyo sasa amevunja kimya chake kuhusu uvumi huo.

Nandy aliweka challenge ya kionjo cha ngoma yake ijayo akiwa anashuka kutoka kwa upande wa dereva kwenye gari lake huku kando yake wakiwa wanaume wawili mapandikizi wakicheza naye.

Ila licha ya kunoga kaitka minenguo yake kwenye kionjo hicho, sehemu kubwa ya mashabiki kwenye komenti zake walionekana kuingia kwa ndani na jicho la kijasusi huku wakizua maswali kuhusu kitumbo cha Nandy.

Nandy alikuwa amevalia kiguo kifupi na kwa hakika kitumbo kama kilionekana kutokea upande wa mbele hadi kuvutia idadi kubwa ya maswali hayo.

Baada ya kuona maswali n imengi, aliamua kumjibu mmoja aliyempongeza kuwa densi ni nzuri lakini pia akaongeza kutaka kujua kama kweli kuna kitu tumboni.

Nandy kwa kujibu alisema kwa utani kwamba kupata mimba ni sehemu ya kazi au tuseme jukumu kuu kwenye ndoa kwani hakuolewa ili kuja kukaa tu na kuangaliana na mume wake.

“Sasa nimeolewa ili nije niangaliane na bwana? Ni kazi kazini,” Nandy alijibu huku akiweka emoji za kucheka.

Itakumbukwa mwaka jana akielekea kanisani kufunga harusi na Billnass, Nandy alikuwa mjamzito na siku chache baadae alijifungua mtoto wa kike ambaye walificha jina lake, jinsi na hata sura.

Hivi majuzi tu alipokuwa akitimiza mwaka mmoja ndipo waliamua kufichua sura na jina lake kwa mashabiki wa mitandaoni kabla ya kumfungulia akaunti ya Instagram.

Kenaya, kama walivyomuita  mpaka sasa ndani ya miezi miwili tayari ashakuwa balozi wa mauzo na akaunti yake inaelekea wafuasi laki 3 kwenye Instagram.