Diamond ambwaga Burna Boy kushinda tuzo ya MTV EMA 2023

Katika kitengo hicho, Diamond alikuwa anamenyana na wasanii kama vile Burna Boy, Asake, wote kutoka Nigeria na mrembo chipukizi kutoka Cameroon, Libianca pamoja na Tyler ICU.

Muhtasari

• Pia ndiye msanii wa kwanza barani Afrika kufikisha watazamaji milioni 900 kwenye YouTube.

• Hafla ya tuzo hizo ilifanyika katika ukumbi wa Paris Nord Villepinte, nchini Ufaransa.

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: Instagram

Msanii wa kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, amefanya urejeo wake kwenye tuzo z MTV EMA mwaka huu kuwa kubwa Zaidi baada ya kuwabwaga wasanii wakubwa barani Afrika kushinda tuzo hiyo kwa mara ya pili katika historia ya maisha yake ya muziki.

Katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa Jumapili, Diamond aliibuka kama msanii bora wa Afrika, Best African Act.

Katika kitengo hicho, Diamond alikuwa anamenyana na wasanii kama vile Burna Boy, Asake, wote kutoka Nigeria na mrembo chipukizi kutoka Cameroon, Libianca pamoja na Tyler ICU.

Diamond Platnumz aliwahi kushinda tuzo mbili za Msanii Bora wa Afrika na mwimbaji Bora Duniani (Afrika/India) kwa usiku mmoja kwenye MTV EMA 2015.

Pia ndiye msanii wa kwanza barani Afrika kufikisha watazamaji milioni 900 kwenye YouTube.

Hafla ya tuzo hizo ilifanyika katika ukumbi wa Paris Nord Villepinte, nchini Ufaransa.

Ili kutazama orodha kamili ya washindi wote, ifuate kwenye kiunganisho hiki cha tovuti rasmi ya MTV EMA.