Harmonize afunguka alivyotapeliwa Ksh 423.8 milioni

Konde Boy alisema kuwa sababu moja ya wasanii wengi kutapeliwa ni ukosefu wa elimu ya kutosha.

Muhtasari

•Staa huyu wa Bongofleva, amekiri alipoteza pesa hizo alizokuwa amepangia kufungua nazo nyumba ya habari ya lebo ya konde.

•"Kuna haja Serekali iweze kutulinda kama wasanii ili kuhakikisha biashara yetu zitafanyika kwa wazi bila ya kutapeliwa," alisema

HARMONIZE/INSTAGRAM
HARMONIZE/INSTAGRAM

Siku chache baada msanii Diamond Platnumz kukiri kutapeliwa shilingi billioni nne za Tanzania  alizoekeza kununua ndege ya kibnafsi, staa mwingine wa bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amefunguka pia na kudai alitapeliwa bilioni saba (Ksh 423.8 milioni).

Staa huyu wa Bongofleva, amekiri alipoteza pesa hizo alizokuwa amepangia kufungua nazo nyumba ya habari ya lebo ya konde.

"Nilikuwa na maono ya kufungua vyumba yva mawasiliano ila nilitapeliwa kwa kuibiwa billioni saba, jambo ambalo ilizima mpango wangu mkuu wa kufungua vituo hivyo vya mawasiliano," Konde Boy alisema wikendi..

Msanii huyo alisimulia hayo kwenye mahojiano ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao alipowasili nchini Kenya kutumbuiza wafuasi wake.

Kwenye mahojiano hayo, msanii huyo alisema kuwa sababu  moja ya wasanii wengi kutapeliwa ni  ukosefu wa elimu ya kutosha.

"Asilimia kubwa ya wasanii hatujaenda shule,wengi tulianzia mtaani kwa kuanza kuimba, nyota zetu zikangaa,tunapopata kiasi kikubwa cha pesa kufanya miamala inakuwa ni tatizo,"alisema.

Harmonize alieleza kuwa kesi hio ya kutapeliwa kiasi hicho cha juu cha pesa ilikabidhiwa kwa serekali na uchunguzi unazidi kufanywa ili aweze kurudishiwa pesa zake ili kurudisha maono yake ya vituo vya mawasiliano.

"Kuna haja Serekali iweze kutulinda kama wasanii ili kuhakikisha biashara yetu zitafanyika kwa wazi bila ya kutapeliwa," alisema