Harmonize ataja sababu ya kufuta tattoo ya Diamond katika mkono wake

"Mimi huchora tattoo kwa upendo wa roho yangu mtu yeyote ninayempenda mimi huchora tattoo ila ninapokerwa na yeyote niliye na tattoo yake mimi huchukua jukumu la kuifuta."

Muhtasari

• Harmonize hata hivyo alisimulia kuwa kuchora Tattoo kwa kabila lao la Makonde ni jambo la kawaida akisema kuwa bibiye yuko na tattoo usoni

Harmonize
Harmonize
Image: Instagram

Staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize asimulia kufuta tattoo ya aliyekuwa bosi wake Diamond Platnumz.

Harmonize hapo awali alikuwa na tattoo ya aliyekuwa  bosi  Diamond yenye mchoro na maadishi "Simba"mkononi  mwake.

Baada ya wanablogu kutaka kujua iwapo msanii huyu bado amehifadhi tattoo ya Diamond kwenye mkono wake aliwaonesha sehemu  ya ngumi kwenye mkono wake kuashiria tayari alikuwa amefuta Tattoo hiyo.

Kwenye mahojiano haya  ya moja kwa moja na wanablogu wa mitandao , bosi huyu  wa Konde Music Worldwide alisema kuwa yeye huchora tattoo kwa anayependa wakati ampamo anakerwa na uchukua hatua  ya kufuta tattoo.

"Mimi huchora tattoo kwa upendo wa roho yangu mtu yeyote ninayempenda mimi huchora tattoo ila ninapokerwa na yeyote niliye na tattoo yake mimi huchukua jukumu la kuifuta na kuisahau,"alisema.

Harmonize hata hivyo alisimulia kuwa kuchora Tattoo kwa kabila lao la Makonde ni jambo la kawaida akisema kuwa bibiye yuko na tattoo usoni.

"Kuchora tattoo si jambo kubwa kwetu mimi mwenye nina tattoo mingi mpaka sijui hesabu zake kwa kabila yetu ya Makonde ni jambo la kawaida,"alisema.