logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwijaku ahusisha masaibu ya Whozu na mikosi ya kushiriki Wasafi Festival ya Diamond

Whozu alipigwa marufuku ya kufanya muziki miezi 6.

image
na Davis Ojiambo

Burudani06 November 2023 - 07:59

Muhtasari


  • • Mwijaku sasa amekuja na dhana tofauti akisema kwamba masaibu yake yametokana na kukubali kushiriki katika msururu wa shoo za Wasafi Festival
Mwijaku na Whozu

Siku moja baada ya baraza la Sanaa Tanzania, BASATA kutoa tamko la kuwafungia wasanii Whozu, Mbosso na Billnass kwa muda wa kati ya miezi 3 hadi 6 na faini ya milioni 3 kwa kuachia video yenye maidhui ya kwenda kinyume na maadili na kanuni za baraza, dhana mbalimbali zimevutwa.

Whozu, ambaye ndiye mwenye wimbo na aliwashirikisha Billnass na Mbosso kwenye remix ya ‘Ameyatimba’ ndiye mwathirika mkubwa katika kichapo hicho cha BASATA.

Whozu alipigwa marufuku ya kutojihusisha kivyovyote vile na kazi ya Sanaa kwa muda wa miezi 6 na kutoa faini ya milioni 3 pesa za kitanzania.

Mwijaku sasa amekuja na dhana tofauti akisema kwamba masaibu yake yametokana na kukubali kushiriki katika msururu wa shoo za Wasafi Festival.

Kwa mujibu wa Mwijaku, Diamond ni mtu mwenye mikosi na mtu yeyote anayevuta kwenye jambo lake moja kwa moja huchukua mgao wa mikosi hiyo.

Pia mtangazaji huyo mwatukaji alikwenda mbele kumpiga vijembe Whozu kwamb masaibu yake yameendelea kwa mfululizo, ikiwa ni hivi juzi tu mamake Wema Sepetu – mpenzi wake alivamia tafrija yao na kuweka wazi kwamba hamtambui kwa vile Wema hakuwahi kumtambulisha nyumbani.

“Kweli ng'ombe wa masikini hazai . Mama mkwe hakutaki huku basata unatakiwa ulipe Milioni 6 . Alafu wakati huo huo ulipe kodi ili usidhalilike . Na show hakuna ndani ya miezi 6 . Nilikwambia kumkumbatia MWAMBINO [Diamond Platnumz] ni mkosi sasa umeamini maneno yangu,” Mwijaku aliandika akiweka picha yake na Whozu Twitter.

Ikitangaza adhabu hiyo, BASATA ilisema kwamba hii si mara ya kwanza kwao kumpa onyo Whozu mara mbili lakini wakasikitika kwamba msanii huyo hakuwahi kuzingatia onyo hizo na hivyo kuvutia adhabu hiyo kali.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved