Kauli ya Diamond baada ya kushinda tuzo ya MTV

Diamond Platnumz aliwahi kushinda tuzo mbili za Msanii Bora wa Afrika na mwimbaji Bora

Muhtasari

• Katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa Jumapili, Diamond aliibuka kama msanii bora wa Afrika, Best African Act.

 

Diamond Platnumz
Diamond Platnumz
Image: Instagram

Msanii  Diamond Platnumz ameshukuru Mungu baada ya kutuzwa kama msanii bora Afrika  kwenye tuzo za MTV EMA mwaka huu.

Kwenye kauli yake  Diamond alishukuru baraza lake muziki kwa bidii yao ambayo imefanikisha ushindi huo kwa ushirikiano mwema na juhudi za kila mmoja.

"Nasifu sana baraza langu la muziki kwa bidii,tumebadilisha muziki wa Tanzania kuwa Bora zaidi barani Afrika Sifa ni kwetu wote,"alisema.

Kwenye taarifa yake Diamond alipongeza Rais wa Tanzania kwa bidii zake kuhakikisha wasanii wanapata mazingira mazuri ya kufanya sanaa bila tatizo.

Katika tuzo hizo zilizotolewa usiku wa Jumapili, Diamond aliibuka kama msanii bora wa Afrika, (Best African Act).

Diamond alikuwa anamenyana na wasanii kama vile Burna Boy, Asake, wote kutoka Nigeria na mrembo chipukizi kutoka Cameroon, Libianca pamoja na Tyler ICU.

Msanii huyo  amefanya urejeo wake kwenye tuzo za  MTV EMA mwaka huu kuwa kubwa Zaidi baada ya kuwabwaga wasanii wakubwa barani Afrika kushinda tuzo hiyo kwa mara ya pili katika historia ya maisha yake ya muziki.

Diamond Platnumz aliwahi kushinda tuzo mbili za Msanii Bora wa Afrika na mwimbaji Bora  kwenye MTV EMA 2015.

Hafla ya tuzo hizo ilifanyika katika ukumbi wa Paris Nord Villepinte, nchini Ufaransa.