Awinja asema anamiliki zaidi ya kamisi 30 zote za kuigiza

Muhtasari

• Zaidi ya uigizaji wake maarufu, Awinja ni muunda maudhui mwenye vipaji vingi anayetambulika sana katika tasnia ya sanaa.

• "Nilianza kujumuisha Kamisi kwa sababu nilitaka kuiga msichana wa mashambani huko kijijini.

• Kamisi ilikuwa vibe enzi hizo na nikazoea tabia hiyo kwa sasa ninamiliki takriban kamisi  30."

Jacky Vike maarufu Awinja
Jacky Vike maarufu Awinja
Image: Instagramu

Muigizaji wa zamani wa kipini cha Papa Shirandula  Jacky Vike, anayejulikana sana kama Awinja, amefunguka na kusema  kuwa ana zaidi ya kamisi 30  ambazo alisema majukumu yazo ni kuigiza.

Zaidi ya uigizaji wake maarufu, Awinja ni muunda maudhui mwenye vipaji vingi anayetambulika sana katika tasnia ya sanaa. 

Awali Awinja alijipatia umaarufu kutokana na kuigiza kama mhudumu wa nyumba katika kipindi maarufu cha Papa Shirandula, jukumu ambalo lilivutia umaarufu wake.

Walakini, talanta yake yenye utani mwingi huenda zaidi ya mipaka ya runinga.na uigizaji, pia amejidhihirisha katika majukumu makuu ya filamu, ikiwa ni pamoja na kuonekana katika filamu maarufu za Kenya kama vile "Nairobi Half-Life" na "Click Click Bang."

Maigizo yake yenye ucheshi yanaendelea kung'aa hasa kwenye filamu za vichekesho na tamthilia za Kenya zilizofanikiwa zaidi.

Akizungumzia mkusanyo wake wa kipekee wa  Kamisis, Awinja alifichua msukumo alionao kwa  nguo hizi ambazo watu wa kizazi cha sasa huichukulia kuwa za kishamba.

"Nilianza kujumuisha Kamisi kwa sababu nilitaka kuiga msichana wa zamani huko kijijini. Kamisi ilikuwa vibe enzi hizo na nikazoea tabia hiyo kwa sasa ninamiliki takriban kamisi  30."alisema.

Alipoulizwa anachagua vipi cha kuvaa, Awinja alisema:

"Kinachoamua ni rangi, ikiwa nimevalia nguo ya kijani kibichi, koti la chini lazima liwe la rangi tofauti."

Licha ya mabadiliko yake kwenye skrini, tabia ya kweli ya Awinja inamvutia sana shabiki wake mkuu ambaye ni mwanawe.

Alisema kwamba mwanawe anapenda sana  jinsi anavyoigiza na kwamba yeye huwa anashabikia sana video zake  mitandaoni.

"Mwanangu husema kwa mshangao, oh Mungu wangu, Mama? Lakini wakati mwingine ananiita Awinja, na wakati mwingine nampata akitazama video zangu kwenye YouTube.”

Wakati wa mahojiano, Awinja pia alichukua muda huo kutafakari kuhusu msiba uliyompata baba yao katika tasnia ya burudani, Charles Bukeko maarufu Papa Shirandula.

Alielezea ugumu wa kukubali  kifo chake na jinsi kilivyoleta familia karibu.

"Ilikuwa ngumu sana kumpoteza baba yetu. Alikuwa ametuleta pamoja, na tulikuwa tukitumia muda mwingi pamoja. Tulihisi kana kwamba hatukuomboleza vya kutosha tangu alipofariki wakati wa janga la Covid-19. Kila kitu kilitokea haraka sana, na hatukukubali hilo.”