KRG Ajibu baada ya kuombwa kuchimbia Wakenya visima kama Mr Beast

Aidha alifichua kuwa hana huruma kwa watu ambao hawako tayari kujiondoa kutoka kwa umaskini.

Muhtasari

• Katika Mahojiano na wanablogu, kwa hasira alisema hata ikiwa yeye ni bilionea, hana wajibu kwa njia yoyote ile kusaidia Wakenya walio na matatizo.

• “Mimi sina deni la Mkenya yoyote, mimi ni mwananchi  pia mwenye kutaka kusaidiwa tu, wewe ulimsaidia aje? mimi si Mungu sina wakfu wowote. mngonjee Mr Beast awafanyie kazi,”

Krg The Don,wakati wa mazungunzo na Mungai Eve
Krg The Don,wakati wa mazungunzo na Mungai Eve
Image: Instagram, Sreengrab

 KRG The Don amewajibu Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wanaomtaka kufuata nyayo za  YouTuba Mr. Beast aliyechimba visima 52 nchini Kenya.

Mashabiki mitandaoni  walimtaka arudishe mkono kwa jamii kwa kufanya miradi ya maendeleo ili kuthibitisha kuwa yeye ni bilionea kama anavyodai.

Katika Mahojiano na wanablogu, kwa hasira alisema hata ikiwa yeye ni bilionea, hana wajibu kwa njia yoyote ile kusaidia Wakenya walio na matatizo.

“Mimi sina deni la Mkenya yoyote, mimi ni mwananchi  pia mwenye kutaka kusaidiwa tu, wewe ulimsaidia aje? mimi si Mungu sina wakfu wowote. mngonjee Mr Beast awafanyie kazi,” Krg alisema.

Msanii huyo, anayejulikana kwa kuwa muwazi na mtindo wake wa maisha, alisema kuwa utajiri wake si kwa ajili ya kufanya nia njema kama bilionea huyo wa Marekani. Aidha alifichua kuwa hana huruma kwa watu ambao hawako tayari kujiondoa kutoka kwa umaskini.

“Pesa ni yangu peke yangu, hata niskie nilalie kama godoro ama nigawie watu wenye nataka nasaidia yule mtu mwenye kutaka, mimi naweza nikakunagalia hapo uko na njaa na mimi nakula na hata sishituki,” alisema.

Krg alikisia kuwa hakuwa anadaiwa chochote na mtu yeyote kwa hivyo hapaswi kukosolewa kwa kutotoa msaada.

“Sina deni la mtu, si hawa ni wale wale tu wakenya wanaoshinda wakitusi wasanii hapa wakiomba msaada. Si ni ukweli? Tena usijisahau eti juu uko na kidogo uende uwasaidie na ikiisha watakuchangia wewe ama wataanzakukuabisha, lazima ufikirie hiyo kwanza,” aliongeza.

Wikendi iliyopita, iliripotiwa kuwa Mr.Beast alidai kuchimba visima 52 nchini kusaidia jamii na pia kujenga madaraja katika maeneo yasiyopitika miongoni mwa miradi mingine ambayo ilikusudiwa kuwasaidia watu wenye maitaji.