Pasta Ezekiel ataka wasanii kuchuguza tunzi zao akirejelea wimbo wa -Moji Short Baba

Moji Short Baba asema kuwa yeye uimba kumtukuza Mungu si mwanadamu

Muhtasari

•Kuimba isiwe ni kwenda tu studio na kutoa ngoma ili kumfurahisha mwanadamu ila kuwe kwa utunzi wa nyimbo zenye mfano mwema na zenye misamiati ya heshima kwa Mungu alisema

Moji Shortbabaa na Pasta Ezekiel
Moji Shortbabaa na Pasta Ezekiel
Image: Facebook, Maktaba

Mchungaji wa kanisa la New life Prayer Center Mavueni Ezekiel Odero amewataka wasanii wa nyimbo za injili kuchunguza utunzi wa nyimbo zao ili ziwe zenye  maadili mema yanayotukuza jina la Mungu.

Kiongonzi huyo wa kanisa alisema hayo wakati wa ibada na wafuasi wake huku akiwaonesha kwa kutoa mfano wa video ya Wimbo wa msanii wa nyimbo za injili  almaarufu Moji Short Baba.

Wimbo wenye maneno "oyooyoo  ayayaaa densi ya kanisa densi ya kanisa," maneno kwenye wimbo yalisema.

"Mnataka kumtukuza Mungu kwa nyimbo kama hizi,hakuna mtu ako na ladha ya miziki kama hizi,hata sauti iwe  inasifiwa sana  hakuna anaye taka kumtukuza Muumba wake Kwa nyimbo hizi,"alisema mchungaji Ezekiel.

Mchungaji huyu aliendelea kutoa kauli yake kwa wafuasi wake akisema kuwa si kuimba tu kunamfuraisha Mungu ila ni yale maneno ya heshima kwa utunzi wa msanii kwa kumtukuza Mungu.

"Kuimba isiwe ni kwenda tu studio na kutoa ngoma ili kumfurahisha mwanadamu ila kuwe kwa utunzi wa nyimbo zenye mfano mwema na zenye misamiati ya heshima kwa Mungu alisema.

Baada ya msanii huyo kufanyiwa mahojiano ya moja kwa moja na mwanablogu kulingana naye wimbo wake ni wa kumtukuza Muumba wake ila si tu kufurahisha wanadamu.

"Mimi huimba kumtukuza kristo si kumfurahisha mwanadamu,"alisema msanii huyo wa Injili.