Vera Sidika ajiondoa katika hafla aliyotarajiwa kutumbuiza pamoja na Ex wake Brown Mauzo

Sidika alisema kwamba hatoruhusu watu kufaidika kutokana na mzozo wa kuachana unaoendelea baina yake na baba watoto wake, Brown Mauzo.

Muhtasari

• "Tafadhali kumbuka kuwa sitahudhuria au kufanya maonyesho katika bustani za mtendaji wa Jami, Mwea,” Sidika alitangaza.

Brown Mauzo na Vera Sidika.
Brown Mauzo na Vera Sidika.
Image: Facebook

Mwanasosholaiti Vera Sidika ametangaza kujiondoa kwake katika hafla ya tafrija ambayo aliratibiwa kutokea huko Mwea kaunti ya Kirinyaga wikendi hii.

Sidika ambaye alikuwa ameratibiwa kutokea kwenye hafla hiyo pamoja na wasanii na watu wengine maarufu Zaidi ya watano kutoka tansia ya burudani humu nchini, alitangaza hilo mapema Alhamisi, siku mbili tu kuelekea siku ya tukio.

Alidokeza kwamba asingeweza kutokea kwa kile alichokitaja kwamba tafrija hiyo imepangiwa pia msanii Brown Mauzo, ambaye ni mpenzi wake wa zamani ambaye wana watoto wawili pamoja.

Vera Sidika alisema kwamba aligundua hafla hiyo inatangazwa kwa njia ambayo wenye tafrija wanataka kutumia mzozo wa kuachana unaoendelea baina yake na Brown Mauzo ili kufaidika, na hivyo hatoweza kukubali hilo kutokea kwa kuhusisha chapa yake na biashara ya aina hiyo.

“Imekuja kwa mawazo yangu kwamba baadhi ya watu binafsi na blogs wanatangaza utendaji fulani kati yangu na Ex kule Mwea. Ningependa kuwafahamisha mashabiki wangu na umma kwa ujumla kuwa aina hii ya utangazaji ni ya kupotosha na ni ya udanganyifu iliyoundwa katika muundo ili kufaidika kutokana na hali ya familia yangu binafsi. Tafadhali kumbuka kuwa sitahudhuria au kufanya maonyesho katika bustani za mtendaji wa Jami, Mwea,” Sidika alitangaza.

Kando na kuandika tamko hilo la kujiondoa, Sidika pia alipakia chapa ya tangazo la hafla hiyo na kweney picha yake akaiweka alama nyekundu ya X lakini pia kwenye jina lake akalifuta na alama yiyo hiyo nyekundu.

Kando na Vera Sidika na Brown Mauzo, wengine ambao wanatarajiwa kutokea kwenye hafla hiyo ni msanii wa rap Khaligraph Jones, MC Gogo, na kundi la Wakadinali.

Katika kile kilichoonekana kama ni hatua ya kumjibu, Brown Mauzo kwa haraka alichapisha picha ya tangazo hilo akiwa amebadilisha picha ya Sidika na ya Kabinga Jr, msichana ambaye alimtangaza kuwa mpenzi wake mpya Jumanne.