Lynne ambwagia sifa kemkem mpenzi wake Eric Omondi

Lynne pia alisema wameongeza ada ya kumona mtoto wao kutoka kwa millioni hamsini hadi sabini.

Muhtasari

•Lynne alikiri upendo mkubwa kwa mpenzi wake na kubainisha kuwa yeye ndiye mwanamke mwenye bahati sana  duniani kwa kuwa kwenye mahusiano na Eric Omondi.

Eric Omondi na mpenzi wake Lynne
Image: ERIC OMONDI//INSTAGRAM

Lynne Njihia , mke wa mchekeshaji Eric Omondi amelimbikizia sifa tele kwa jinsi anavyotumikia familia yake kwa upendo na furaha wakati wanapomlea mtoto wao mchanga wa miezi mitatu,wayempa jina Kaylar.

Kwenye mahojiano ya moja kwa moja, Lynne alikiri upendo mkubwa kwa mpenzi wake na kubainisha kuwa yeye ndiye mwanamke mwenye bahati sana  duniani kwa kuwa kwenye mahusiano na Eric Omondi.

"Haya mapenzi sitatoka kamwe ndio yenye upendo mwingi na furaha," alisema Lynne.

"Najivunia sana kuwa mwanamke mwenye bahati sana  duniani napedwa sana, japo kuwa Eric amependa mtoto wake Kaylar kuniliko, hiyo ndio furaha ya maisha yangu,"alisema.

Aidha, alifichua maelezo kuhusu safari yao nje ya nchi ambapo alisimulia kuwa wapanga kumtembeza mtoto wao mchanga kwani walimchukulia pasipoti akiwa na umri wa wiki mbili.

"Mtoto wetu anafaa kutembea kwani ni mtoto wa Rais wa vishekesho 'malkia Kaylar', kila stakabadhi ya kusafiri zimo, tupanga kumtembeza mataifa ya nje,"alisema.

Kwenye mahojiano hayo, Lynne alisema kuwa wameongeza pesa za kuona mtoto wao kutoka kwa millioni hamsini hadi sabini.

"Venye Rais Ruto ameongeza bei ya bidhaa nchini, pia sisi tumeogeza bei kwa yeyote yule anataka kumuona mtoto wetu hadi milioni sabini,"alisema.