Hatimaye mwanawe Diamond na Tanasha ameanza shule, karo zaidi ya milioni 40

Mama Dangote aliandika kwamba Diamond Platnumz ndiye alirauka alfajiri mapema kumpeleka mwanawe shule,

Muhtasari

• Kwa mujibu wa blogu moja kutoka nchini humo ambaye ilidai kwamba shule hiyo ipo katika maeneo ya karibu na ofisi zao,.

Naseeb Jr
Naseeb Jr
Image: Instagram

Naseeb Junior, mwanawe Diamond na Tanasha Donna kutoka Kenya hatimaye ameanza safari yake ya kusoma nchini Tanzania.

Mtoto huyo ambaye anatajwa kuwa ndiye pendwa Zaidi kati ya watoto wanne wa Diamond kwa muda sasa amekuwa akionekana na bibi yake, Mama Dangote nchini Tanzania na imefichuliwa kwamba hatimaye wameamua kumuanzishia elimu yake ya msingi nchini humo.

Katika video ambayo Mama Dangote alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Naseeb Jr alionekana amevalia sare za shule katika baraza la shule ya kifahari huku akiwa anadeka.

Mama Dangote aliandika kwamba Diamond Platnumz ndiye alirauka alfajiri mapema kumpeleka mwanawe shule, akionesha furaha kwamba mrithi wa mwanawe naye ameanza safari ya kuyabukua mabuku.

“Kweli Tom kaka amekuwa.. Atimae Naseeb kichwa @diamondplatnumz 🦁 anaamka asubuhi kumpeleka mtoto @naseeb.junior shule… 🤲” aliandika Mama Dangote.

Kwa mujibu wa blogu moja kutoka nchini humo ambaye ilidai kwamba shule hiyo ipo katika maeneo ya karibu na ofisi zao, walifichua kwamba karo ya kumuingiza mtoto kama Naseeb Jr si chini ya shilingi milioni 40 za Kitanzania.

Blogu hiyo ilisema kwamba shule hiyo iko katika maeneo ya Mbezi Beach na kama si kuongoza kwa gharama ya juu ya karo basi ni miongoni mwa shule zenye gharama ya thamani iliyotukuka.