Juliana Kanyomozi azungumzia madai kuwa mtoto wa Museveni ni baby daddy wake

Alisema anapendelea maisha ya kibinafsi. Wamekuwa pamoja kwa miaka 7.

Muhtasari

• "Niko katika sehemu ya furaha sana hivi sasa na sijisikii kuishiriki hadharani, lakini wao (mashabiki) wanakataa kuelewa," alisema.

Juliana Kanyamozi
Juliana Kanyamozi
Image: Instagram

Mwanamuziki wa Uganda Juliana Kanyomozi amekumbana na tetesi kuhusu utambulisho wa babake mtoto tangu kujifungua mtoto wake wa pili.

Mtoto wake wa pili Taj, mvulana, alizaliwa mnamo 2020.

Alizungumza kuhusu yeye na mwenzi wake kufurahishwa na kuzaliwa kwa Taj. Hakutaja na hadi leo hajawahi kufichua yeye ni nani.

Hili mara zote limeacha nafasi kwa uvumi, huku wanamtandao wakielekeza mtoto wa Rais Yoweri Museveni kama baba mtoto.

Mwana huyo, Jenerali Muhoozi Kainerugaba si mgeni kwa Wakenya. Alikashifu taifa kwa maoni kuhusu uwezekano wa kutwaa jiji katika mfululizo wa tweets za uchochezi. Wakati huo alikuwa kiongozi wa Jeshi la Uganda.

Mnamo Jumapili, Nov 12, Juliana aliangaziwa kwenye msimu wa 2 wa Mazungumzo ya Tusker Malt yanayoendelea nchini Uganda ambapo alionyesha kutofurahishwa na uvumi huo.

"Siwezi hata kueleza jinsi nilivyohisi. Niliona ni heshima sana kwangu na kwa Mwana wa Kwanza wa taifa. Sikuwa nimewahi kukutana naye kimwili maishani mwangu...nilikutana naye hivi majuzi huko Soroti. Kwa hivyo nikaona ni mbaya."

"Watu hukimbia na kile kinachoweza kuleta likes, shares, na attention. Watatengeneza vitu ili ku-trend tu, lakini wasichotambua ni kwamba mambo hayo yanaathiri watu katika maisha yao ya kibinafsi.. Nina familia; mwanangu ana baba mzuri na anasoma mambo hayo,” aliongeza.

Alisema anapendelea maisha ya kibinafsi. Wamekuwa pamoja kwa miaka 7.

"Niko katika sehemu ya furaha sana hivi sasa na sijisikii kuishiriki hadharani, lakini wao (mashabiki) wanakataa kuelewa," alisema.

Kuzaliwa kwa Taj kulikuwa miaka sita baada ya kumpoteza mwanawe mwingine Keron Raphael Kabugo mnamo 2014. Keron alifariki akiwa amelazwa katika hospitali ya Nairobi baada ya kuugua pumu kwa muda mrefu.

Alihofia hataweza kuwa mama tena kufuatia majaribio kadhaa bila mafanikio.

“Katika suala la uzazi huwa namuachia Mungu, watu walikuwa wakiniuliza lini utampata mtoto mwingine, na mimi nilikuwa nawaambia kuwa namuachia Mungu. Anapoamua nipate mtoto mwingine, basi nitapata mtoto mwingine na ikawa hivyo,” mwimbaji huyo alisema kwenye YouTube.