Zari ajibu kwa nini muda wote Tiffah ana muonekano mmoja tu wa nywele kichwani

"Kwa vile mliamua kulifanya jambo la kwenu, natumai sasa mmepata majibu nyinyi wajinga,” Zari alimaliza.

Muhtasari

• “ ‘Ooh si ubadilishe nywele za binti yako anaonekana vibaya na wewe muda wote uko vizuri..’ inakuhusu?" Zari alianza.

Zari na bintiye Tiffah
Zari na bintiye Tiffah
Image: Instagram

 Baada ya kukerwa na maswali ya mashabiki wake kuhusu kile walihisi ni kumtelekeza bintiye kwa mionekano na mitindo mizuri ya ususi, hatimaye mfanyibiashara Zari amejibu kwa ukali.

Kupitia video fupi aliyoipakia katika ukurasa wake wa Snappchat, Zari aiamua kuvunja kimya kuhusu watu kumuuliza mbona hajawahi mbadilisha bintiye Tiffah muonekano wa nywele kichwani.

Zari alisema kwamba aliamua kumuacha bintiye kujiburudisha maisha yake kama mtoto wala hayuko mitandaoni ili kuwafurahisha watu kwa kumpa bintiye muonekano mpya wa nywele kila baada ya siku chache.

Aidha alisema kwamba sababu inayomfanya Tiffah kuishi na mtindo huo mmoja tu wa kusuka nywele muda wote ni kutokana na kwamba nchini Afrika Kusini sasa hivi wako katika majira ya joto na mtoto huyo shuleni muda wote anashinda kwenye bwawa la kuogelea jambo ambalo akimpa mtindo mpya maji yatauharibu.

“ ‘Ooh si ubadilishe nywele za binti yako anaonekana vibaya na wewe muda wote uko vizuri..’ inakuhusu? Nchini Afrika Kusini sasa hivi ni majira ya joto. Inaweza kuwa siku 3 mfululizo wanaogelea shuleni baada ya chakula cha mchana. Akifika nyumbani pia tuna bwawa la kuogelea, anafanya vile vile. Niliamua kumuacha binti yangu kujienjoy kama mtoto…”

“Sitaki yeye aonekane mkamilifu kwa jamii ya mitandaoni eti kisa mamake anafanya hivi na yeye afanye kwa sababu nataka kuwafurahisha nyinyi wapumbavu. Yeye ni mtoto na anafurahia majira ya joto na anaogelea akiwa na nywele za kiafrika namna hiyo, ambayo kwa kawaida ni muonekano mzuri,” alisema Zari.

Hata hivyo, Zari alisisitiza kwamba kuacha binti yake kudumu na mtindo mmoja wa kusukwa kuna maana kwamba hamuandai vyema kwa ajili ya kuhudhuria masomo shuleni.

Mama huyo wa watoto watano ambaye pia ni mzazi mwenzake na Diamond Platnumz aliwakoromea vikali wanaochukulia suala la familia yake kuwa lao na kulivalia njuga akisema kwamba mpaka hapo katika maelezo hayo, basi anatumai walishapata majibu mwafaka.

“Asubuhi anapoondoka kwenda shuleni, huwa anaandaliwa vizuri na kutokea maridadi kwa ajili ya kukimbia shuleni. Nywele yake huwa imefanywa vizuri na anakwenda shuleni, sawa? Kwa vile mliamua kulifanya jambo la kwenu, natumai sasa mmepata majibu nyinyi wajinga,” Zari alimaliza.