Burna Boy atishia kuajiri wanasheria 100 ili kuwashtaki wanablogi wanaoandika habari zake

"Hizi pesa ninazotaka kuwapa watu kwenye blogi kwa wakati huo, ni kama kusema na kutoa kama mawakili 100 sasa." Burna Boy alisema.

Muhtasari

• Hii ilikuja baada ya vyombo vya habari kuripoti kwamba msanii huyo aliwahi kataa shoo ya hela ndefu jijini Dubai.

Burna Boy
Burna Boy
Image: Instagram

Nyota wa Afrobeats, Damini Ogulu, almaarufu Burna Boy, ametishia kuajiri mawakili 100 ili kuwashtaki wanablogu wa Nigeria wanaozidi kuandika kila kitu kuhusu maisha yake na mitikasi yake katika tasnia ya muziki.

Msanii huyo aliyeshinda tuzo ya Grammy ambaye alifahamisha haya kwenye chapisho kupitia ukurasa wake wa X siku ya Jumatano alisema kuwa anasukumwa kufanya hivyo.

"Hizi pesa ninazotaka kuwapa watu kwenye blogi kwa wakati huo, ni kama kusema na kutoa kama mawakili 100 sasa. Lakini najua niseme kwamba kila mtu anahangaika na kuniumiza ikiwa nitaendesha bati kama hilo. Kwa nini unanisukuma?” aliuliza.

Radiojambo.co.ke inaripoti kuwa hii inakuja karibu wiki mbili baada ya kutoa pesa kwa wanablogu wa Nigeria kuacha kuripoti kumhusu.

Kulingana naye, ingawa hakuwahi kulipa chombo chochote cha habari kutangaza chapa yake, alikuwa tayari kufanya hivyo ili asitangazwe.

“Hadi lini. Hizi zote za instablog, PulseNg e.t.c beg zinafanya mkutano wote kisha niamue ni kiasi gani nitakupa zote unasahau jina langu kabisa. Najua sema sijawahi kulipa una kabla kwa hivyo nasema fanya niendeshe mwishowe. Nawasalimu ndugu zangu!” alikuwa amefichua.

Hii ilikuja baada ya vyombo vya habari kuripoti kwamba msanii huyo aliwahi kataa shoo ya hela ndefu jijini Dubai baada ya kutaarifiwa kwamba asingeweza kuingia jukwaani na bangi yake.

Burna Boy ni mmoja wa wasanii ambao hawaoni aibu kuvuta sigara zao hadharani tena wakiwa wanatumbuiza jukwaani.

Itakumbukwa pia kwa wakati mmoja msanii Ed Sheeran alisema kwamba alishangazwa na kiasi cha bangi ambacho msanii huyo anatumia.

Sheeran alisema kwamba katika maisha yake ya muziki, hajawahi kutana na mtu anayependa kuvuta bangi wakiwa kazini kama Burna Boy.