Wiki chache baada ya kupata mapacha, mkewe Davido ajitokeza kwenye shoo na kunengua

Mama huyo, akiwa amevalia gauni dogo la Louis Vuitton lililounganishwa na sneakers, alicheza rekodi ya mume wake, ‘Unavailable.’

Muhtasari

• Mama huyo, akiwa amevalia gauni dogo la Louis Vuitton lililounganishwa na sneakers, alicheza rekodi ya mume wake, ‘Unavailable.’

Wiki chache baada ya kuwakaribisha mapacha na mumewe, msanii wa Nigeria Davido, Chioma Rowland, katika video inayovuma sasa, alionyesha ustadi wake wa kucheza kwenye Tamasha la AWAY huko Atlanta lililoandaliwa na mumewe Davido.

Mama huyo, akiwa amevalia gauni dogo la Louis Vuitton lililounganishwa na sneakers, alicheza rekodi ya mume wake, ‘Unavailable.’

Wanandoa hao, ambao walipoteza mtoto wao wa kiume, Ifeanyi, kufuatia ajali iliyotokea nyumbani kwao mnamo 2022, walithibitisha kuzaliwa kwa mapacha wao mnamo Oktoba 2023.

Davido akifichua kwa mara ya kwanza hisia zao jinsi zilivyokuwa baada ya kugundua kwamba walikuwa wanatarajia mapacha, alisema wote walikuwa wanatetemeka kwa kuchanganyikiwa na kwa saa kadhaa wote walibaki kimya midomo wazi.

“Mimi na mke wangu tulipogundua, tulikuwa tunatetemeka na ilikuwa mwezi huo huo. Mwanangu alifariki mwaka jana Oktoba, mke wangu alijifungua mwaka huu Oktoba hivyo ni mambo.” Alisema.

Msanii huyo alisema kwa furaha kwamba hatokaa kumlaumu Mungu kwa kile kilichotokea kufuatia kifo cha aliyekuwa mrithi wake Ifeanyi Oktoba mwaka jana, akisisitiza kwamba walipoteza mwana Oktoba na mwaka mmoja baadae – tena mwezi Oktoba wakabarikiwa na fungu mara mbili.

Baada ya kumzalia mapacha, Davido alidaiwa kumzawadi mkewe zawadi mbali mbali ikiwemo mikoba ghali na nyumba nchini Marekani.