Jinsi mkasa wa 'Online dating' uliwakuta marapa 2 wa TZ wakiwa Media Tour jijini Nairobi

Wasanii hao walisema kwamba kilichowakuta katika chumba chao cha kulala ni simulizi ya siku nyingine lakini mmoja wao ni kama alimezwa na ulevi na kulazimika kukifanya.

Muhtasari

• Lakini kwa kisa hiki ambacho alikihadithia, ni tukio la kweli ambalo liliwakuta ndani ya jiji la wajanja – Nairobi – wakiwa katika media tour ya kutambulisha kazi zao za Sanaa

Roma na Stamina.
Roma na Stamina.
Image: Facebook

Rapa wa Tanzania ambaye kwa sasa yuko uhamishoni nchini Marekani, Roma Mkatoliki amesimulia kisa ambacho kilimkuta kwa wakati mmoja jijini Nairobi Kenya akiwa na rapa mwenzake Stamina Shorwebwenzi.

Roma kupitia ukurasa wake wa X, katika siku za hivi karibuni amekuwa ni msimulizi mzuri sana ambaye anahadithia visa vya kweli na vingine vya kubuni.

Simulizi hiyo pia aliipakia katika mtandao wake wa Instagram.

Lakini kwa kisa hiki ambacho alikihadithia, ni tukio la kweli ambalo liliwakuta ndani ya jiji la wajanja – Nairobi – wakiwa katika media tour ya kutambulisha kazi zao za Sanaa.

Roma alisema kwamba waliingia katika hoteli na kukodisha chumba na hapo ndipo mawazo na fikira za uzembe ziliwaingia kiasi kwamba wakaingiwa na majaribu ya kuwaza mapenzi.

“Tulienda Nairobi na mwanangu Stamina kufanya media Tour. Tukiwa Apartment tulikaa kinyonge sana. Host wetu kuna maunyama sana, hakuwa anatisha…” Roma alianza simulizi.

Alisema kwamba walitiana hamnazo na kuipakua app ya Tinder ambayo inajihusisha na kuwaunganisha watu wawili kimapenzi kupitia njia za kimitandao.

Baada ya kuipakua app ile, walianza kutafuta warembo ambao wako karibu na chumba chao na kwa bahati nzuri walipata mmoja na kuwasiliana naye hadi kumpa maelekezo ya walipo.

Lakini mrembo huyo alipofika, wote walibaki midomo wazi …

“Tukafanikiwa kuongea na mmoja tukampa location akasema yuko njiani tumpe dakika 30. Aliyeibuka na tuliyemuona kwa picha ni vitu viwili tofauti. Kwanza alionekana mzee halafu ni kama ametumika sana sura kama ya babu,” Roma alisema.

Lakini kwa kuhofia usalama wao na wapo mbali na nyumbani, ilibidi tu wajitie moyo kuzungumza naye kwani hawakutaka kuzua rabsha kwa kumkataa papo hapo.

Kwa kumalizia katika njia ya kujinasua kwenye mtego, Roma alisema kwamba Stamina alimalizia kwenda na yule mwanadada, kitu ambacho kilimanya [Roma] ajisi kabisa kwamba mwenzake labda alikuwa anaongozwa na ulevi kichwani.