Azziad Nasenya asimulia Jinsi alivyokabiliana na msongo wa mawazo

Kwa sasa, Azziad sio tu mshawishi; pia anafanya kazi kwenye redio na ana kampuni zingine anazotangaza bidhaa.

Muhtasari

• Akizungumza katika mahojiano na Dr Ofweneke,  Azziad alisema kuwa mawazo mengi ya kujitoa uai yalimjia  baada ya video zake kuvuma mitandaoni alizoshiriki katika ngoma ya Mejja na Femi One ‘Utawezana’.

•nilijaribu kuvumilia nikashindwa,,,nakumbuka nilikuwa peke yangu,,nilikuwa nalia,nikatoka nje kwenye balkoni,nikatazama chini na nikaongea na Mungu wangu nikamuuliza,je Mungu hapa ndipo ulitaka niende?

Azziad Nasenya
Azziad Nasenya
Image: INSTAGRAM

Sosholaiti wa Kenya na mshawishi Azziad Nasenya amezungumzia jinsi alivyokabiliana na hali ngumu ya msongo wa mawazo ambayo ilimletea mawazo ya kujitoa uai.

Akizungumza katika mahojiano na Dr Ofweneke,  Azziad alisema kuwa mawazo mengi ya kujitoa uai yalimjia  baada ya video zake kuvuma mitandaoni alizoshiriki katika ngoma ya Mejja na Femi One ‘Utawezana’.

Nasenya alisema kuwa awali watu walikuwa wanamchukulia vizuri baada ya kutazama ngoma hiyo ila baada ya siku moja mjadala ukabadilika na akawa anakashifiwa na baadhi ya mashabiki jambo ambalo alisema lilikuwa chanzo cha mawazo hayo.

Alisema  kuwa wakati huo alikuwa akiishi katika ghorofa ya 4 ambapo alitoka nje na kuwazia kujitoa uai ila maombi yake kwa Mungu yakazidi mawazo hayo mabaya.

“Maoni kuhusu video hiyo yilibadilika baada ya siku moja na nusu,na nikaanza kupokea ukosoaji kutoka kwa baadhi ya mashabiki,,nilijaribu kuvumilia nikashindwa,,,nakumbuka nilikuwa peke yangu,,nilikuwa nalia,nikatoka nje kwenye balkoni,nikatazama chini na nikaongea na Mungu wangu nikamuuliza,je Mungu hapa ndipo ulitaka niende? Alisimulia.

Hata hivyo alirudi kwa nyumba kwani alitafakari kuwa hata akiwazia kujitoa uai hakuna atakayejali na hivyo kuachana na wazo hilo .

Aliezeza jinsi alivyopokea ushauri kutoka kwa watu twake wa karibu ambao walimpa tumaini na hatimaye akafaulu kukabiliana na hofu hiyo na kukubali kwamba si kila mtu angependa anachofanya.  

Kwa sasa, Azziad sio tu mshawishi; pia anafanya kazi kwenye redio na ana kampuni zingine anazotangaza bidhaa.