logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Baba Levo kuuza mali zake zote kupambana na waliomtapeli Diamond bilioni 4 za helikopta

Diamond alisema alitapeliwa bilioni 4 za kitanzania katika mchakato wa kununua ndege.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 December 2023 - 10:59

Muhtasari


  • • Hata hivyo alisisitiza kwamba shil9ngi bilioni 4 si kitu kwa Diamond japo kwamba kuibiwa kwazo kulififisha ndoto yake tena kununua ndege ya kibinafsi.
Diamond na Baba Levo

Chawa na mtunza siri mkuu wa Diamond Platnumz, Baba Levo ameonesha kwamba bado kitendo cha Diamond kutapeliwa shilingi za kitanzania Bilioni 4 kimasihara katika mchakato wa kununua ndege ya kibinafsi bado kinamuumiza sana.

Levo katika kipindi cha Refresh kwenye Wasafi, alibainisha kwamba yeye anazidi kumshawishi na kumpa msukomo Diamond kwamba wasije wakaacha suala hilo likaenda hivi hivi hata kama liko mikononi mwa sheria.

Alifichua kwamba anafikiria kupiga debe mali yake yote ili kuanza kuhangaika kumtafut mtapeli huyo aliyemharibi ndoto ya kupanda ndege ya kibinafsi.

“Kuna watu ambao wameshamtendea mabaya Diamond Platnumz, wamechukua Zaidi ya bilioni 4 ambazo tulikuwa tunategemea tupande na sisi private jet ya mzee wake, Diamond ni mzee wangu, sasa hiyo ndoto imeuawa. Sasa nasema hivi, kama ni mswahili tutaonyeshana hapa hapa Kiswahili na wale ambao ni wazungu tutawafuata huko,” alisema akijaribu kujichanganya katika lugha ya Kiingereza.

Hata hivyo alisisitiza kwamba shil9ngi bilioni 4 si kitu kwa Diamond japo kwamba kuibiwa kwazo kulififisha ndoto yake tena kununua ndege ya kibinafsi.

“Diamond ndio msanii wa Tanzania tajiri kwa hiyo hamkuchukua chochote, tutawapata na mtaona chenye tutawafanyia, tutaona. Bilioni 4 ni kama anayeramba asali kwenye pipa, utamalizaje asali kwa kuiramba? Niko tayari niuze vitu vyangu vyote, magari na hata nyumba nitafute hela niende huko kwenye mwizi huyo yuko,” aliongeza.

Mwezi mmoja uliopita, Diamond alifichu kwamba mashabiki wake hawajapata kuona akiruka na ndege yake ya kibinafsi kama alivyowaahidi mwaka jana.

Alifichua kwamba alitapeliwa kiasi hicho kikubwa cha hela lakini pia akasema kuwa mamlaka husika zilikuwa zinalifanyia kazi suala hilo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved