Burna Boy ataka watu kuacha kumlinganisha na Wizkid na Davido, "Sijawafikia hata kidogo"

Katika tasnia ya muziki ya Nigeria, "Big 3" wanajulikana kuwa Wizkid, Davido, na Burna Boy kutokana na mafanikio yao kwenye jukwaa la kimataifa kama wasanii wa Afrobeats

Muhtasari

β€’ Aliongeza kuwa wapo wakubwa 2 tu akiwemo Wizkid na Davido na yeye sio sehemu yao

Wizkid, Burna Boy na Davido.
Wizkid, Burna Boy na Davido.
Image: Facebook

Msanii wa Afrobeats anachukuliwa kama mmoja mwenye mafanikio makubwa kutoka nchini Nigeria, Burna Boy amewataka mashabiki wake kuacha kumlinganisha kimafanikio na kimuziki na wenzake Wizkid na Davido, akisema kwamba yeye bado hajawafikia wababe hao wawili hata kidogo.

Mshindi huyo wa Grammy alizungumza haya katika video moja ambayo inamuonesha akiwa anatumbuiza jukwaani kwa mashabiki wake ambapo alisitisha tumbuizo na kuamua kulizungumzia suala la mashabiki wake kumweka mbele ya Davido na Wizkid kwa ulinganisho.

Katika tasnia ya muziki ya Nigeria, "Big 3" wanajulikana kuwa Wizkid, Davido, na Burna Boy kutokana na mafanikio yao kwenye jukwaa la kimataifa kama wasanii wa Afrobeats.

Akijibu dai hilo la Big 3 linalovuma miongoni mwa mashabiki wa muziki nchini Nigeria, Burna Boy katika onyesho hilo alikashifu msemo uliozoeleka akidai kuwa yeye si miongoni mwa wanaoitwa Big 3.

Aliongeza kuwa wapo wakubwa 2 tu akiwemo Wizkid na Davido na yeye sio sehemu yao.

Akijisifu zaidi, Burna Boy alisema baada ya wawili hao, pengine ndio mashabiki wanaweza anza kufikiria kuhusu Burna Boy - akimaanisha kwamba yuko kwenye kiwango tofauti kabisa, tofauti na Wizkid na Davido na wapenzi wa Muziki hawapaswi kumpeleka kwenye ushindani usio wa lazima na Big 2.

Burna Boy alisema; "Wakati ujao mtu yeyote atakuambia juu ya kitu chochote kinachoitwa 'big 3', mwambie kuna 'big 2' tu halafu, kuna Burna Boy."