RIP: Dadake Pasta Kanyari auawa kinyama katika mzozo wa kimapenzi

Polisi walikuta mwili wa sosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 24 kwenye dimbwi la damu akiwa na kisu, kondomu iliyotumiwa, vifaa vya kupima virusi vya UKIMWI vilivyotumika pamoja na chupa ya pombe

Muhtasari

• Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wawili hao walikuwa wamepanga nyumba hiyo kwa kulala usiku kabla ya kila kitu kugeuka kuwa mbaya.

Starlet Wahu, dadake Pasta Kanyari
Starlet Wahu, dadake Pasta Kanyari
Image: X

Dadake Mchungaji Victor Kanyari, Starlet Wahu, ameripotiwa kuuawa katika kile kilichoripotiwa kuwa ni mzozo wa kimapenzi ndani ya nyumba ya kukodisha ya AirBnB mtaani South B, viungani mwa jiji kuu la Nairobi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Mshukiwa ambaye alionekana akiandamana na marehemu kwenye Airbnb kwenye picha za CCTV tangu wakati huo amekamatwa na yuko chini ya ulinzi wa polisi.

Polisi waliitwa kwenye eneo la tukio na meneja wa ghorofa na walipofika, walilazimisha kuingia ndani ya nyumba hiyo kwani ilikuwa imefungwa kwa nje.

Polisi Walikuta mwili wa sosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 24 kwenye dimbwi la damu akiwa na kisu, kondomu iliyotumiwa, vifaa vya kupima virusi vya UKIMWI vilivyotumika pamoja na chupa ya pombe, chanzo kimoja cha habari kiliripoti.

Mshukiwa aliyetambulika kwa jina la John Matara alikamatwa na kwa sasa anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Industrial Area kwa siku 21 huku uchunguzi wa mauaji hayo ya kikatili ukiendelea.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wawili hao walikuwa wamepanga nyumba hiyo kwa kulala usiku kabla ya kila kitu kugeuka kuwa mbaya.

Chanzo cha kitendo hicho kiovu hakijajulikana, lakini polisi wamemkamata mhusika John Matara.

Wakenya kutoka matabaka mbalimbali wameomboleza Starlet Wahi huku wengi wakitaka Haki kutendeka katika kesi ya mauaji.