Davido ampa mwanawe zawadi ya shilingi milioni 1.5 kwa ujasiri wa kung'olewa jino (video)

Hata hivyo, itakumbukwa kwamba bintiye Hailey ni mtoto ambaye alizaa nje ya ndoa na mama mwingine na wala si mtoto wake na Chioma.

Muhtasari

• Itakumbukwa mwezi Oktoba mwaka jana, Davido pia aliripotiwa kumpa mkewe zawadi ya nyumba nzuri nchini Marekani kama zawadi ya kumzalia watoto mapacha.

Davido na bintiye.
Davido na bintiye.
Image: Instagram

Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Davido amewashangaza watumiaji wa mtandao baada ya kumzawadia bintiye dola elfu 10 kwa kung'oa meno yake.

Binti yake Hailey sasa ana umri wa miaka mitano na atakuwa na umri wa miaka sita Mei 2024.

Katika video ya kupendeza ya baba na binti inayosambaa mtandaoni, Davido anaonekana akiwa amembeba bintiye Hailey huku wakishiriki kwa muda.

"Agiza mtoa jino nimpe Dola 10,000," Davido alisema.

Mwimbaji huyo wa Tuzo ya Grammy anajulikana kuonyesha upendo wa umma kwa watoto na familia yake kwa kuchapisha picha zao za kupendeza zikiambatana na jumbe za kuchangamsha moyo.

Itakumbukwa mwezi Oktoba mwaka jana, Davido pia aliripotiwa kumpa mkewe zawadi ya nyumba nzuri nchini Marekani kama zawadi ya kumzalia watoto mapacha.

Msanii huyo alipata bahati ya kubarikiwa na mapacha mwaka mmoja tu baada ya kumpoteza aliyekuwa mrithi wake na mkewe Chioma, Ifeanyi.

Hata hivyo, itakumbukwa kwamba bintiye Hailey ni mtoto ambaye alizaa nje ya ndoa na mama mwingine na wala si mtoto wake na Chioma.

David Adedeji Adeleke OON (amezaliwa Novemba 21, 1992), ambaye kitaaluma anajulikana kama Davido, ni mwimbaji wa Nigeria, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa rekodi lebo.

Anachukuliwa sana kama mmoja wa wasanii muhimu wa Afrobeats wa karne ya 21.

Anasifika pamoja na Burna Boy na Wizkid kwa kutangaza muziki wa afrobeti duniani kote.