logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Epuka njia za mkato maishani" - Willy Paul awashauri wanawake

“Wanawake, kuhudhuria katika kila tafrija hivi si lazima; kama huna pesa, kaa tu nyumbani.."

image
na Davis Ojiambo

Burudani07 January 2024 - 09:21

Muhtasari


  • • Miezi 6 iliyopita, Willy Paul alishauri wanaume kukaa mbali na wanawake waliovunjika kwa kile alichotaja kuwa 'wana rutuba sana'.
Pozee atoa usemi wake kuhusu muziki wa Kenya kudorora.

Mtumbuizaji wa Kenya Willy Paul amewashauri wanawake kujiepusha na ‘njia rahisi’ maishani na badala yake watafute riziki ya uaminifu.

Katika chapisho la kina la mtandao wa kijamii, msanii huyo wa Kenya alisema kuwa kutumia njia za mkato kunaweza kuonekana kuwa kishawishi, kuna manufaa ya muda mfupi na kunaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kifo.

Aidha aliwashauri wanawake dhidi ya shinikizo za kijamii zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Wanawake, kuhudhuria katika kila tafrija hivi si lazima; kama huna pesa, kaa tu nyumbani. Epuka marafiki wanaokushawishi kwa ofa kama vile kubebwa kwenye gari. Usiruhusu shinikizo la mitandao ya kijamii likuathiri. Nenda huko na ufanye bidii kwa njia sahihi. Kuchagua njia za mkato kutafupisha maisha yako. Hujachelewa sana kuanza upya,” pozee aliwashauri.

Willy Paul anatoa matamshi haya saa chache baada ya habari kusagaa mitandaoni kwamba mwanasosholaiti Starlet Wahu ambaye ni dadake mchungaji Victor Kanyari aliuawa kinyama na mwanamume ambaye walikisiwa kuingia naye katika nyumba moja ya Airbnb mtaani Soith B.

Wahu ambaye amekuwa akionesha maisha yake ya kitajiri mitandaoni alipatikana ameuawa kwa kisu ndani ya nyumba hiyo.

Miezi 6 iliyopita, Willy Paul alishauri wanaume kukaa mbali na wanawake waliovunjika kwa kile alichotaja kuwa 'wana rutuba sana'.

"Kaa mbali na wanawake waliovunjika. Wamezaa sana,” aliandika msanii huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kufuatiwa na emoji ya kucheka.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved