• “Ukweli usemwe. Kufanana ni ajabu, pozi, soketi za macho, midomo na sura ya uso 100% Wang'ombe! Lakini je, tunasema?” Stacey Waweru aliradidi.
• “Huyu ni ndugu yako buana” Dennis Mutembei alimwambia.
Mchekeshaji Henry DeSagu amevunja kimya chake siku chache baada ya Wakenya wengi kumhusisha na kuwa na uhusiano wa kiukoo na mshukiwa wa mauaji ya dadake Pasta Kanyari, mwanasosholaiti Starlet Wahu.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, DeSagu kwa ucheshi alifutilia mbali kuhusishwa na jamaa huyo kwa jina la John Matara ambaye picha zake zimekuwa zikienezwa katika mitandao ya kijamii tangu wikendi kisa cha kushukiwa kumuua tarlet Wahu kilipogonga vichwa vya habari.
DeSagu alisema kuwa hana uhusiano wowote na Matara, licha ya kuwa wengi wamekuwa wkaizua utani kuwa wawili hao ni kama reale kwa ya pili.
“Sina uhusiano na John Matara. Any such Hullabaloo associating me with him should be disregarded, discombulated and disconfisured with utmost hubwatete,” DeSagu alisema.
Hata hivyo, mashabiki wake walishikilia msimamo wao kuwa DeSagu na Matara ambaye kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi wanafanana kwa asilimia kubwa haswa kwenye sura za usoni.
“Ukweli usemwe. Kufanana ni ajabu, pozi, soketi za macho, midomo na sura ya uso 100% Wang'ombe! Lakini je, tunasema?” Stacey Waweru aliradidi.
“Huyu ni ndugu yako buana” Dennis Mutembei alimwambia.
“labda nurses wenye walikuwa kuwa ward walete ukweli,,,, huyu sio just brother😂😂 ni twin”Joy Joy the Girl.
“𝑀𝑛𝑎𝑓𝑎𝑎 𝑘𝑢𝑒𝑛𝑑𝑎 𝑚𝑘𝑎𝑓𝑎𝑛𝑦𝑒 𝐷𝑁𝐴 𝑘𝑤𝑎𝑛𝑧𝑎 𝑐𝑜𝑠 𝑟𝑒𝑠𝑒𝑚𝑏𝑙𝑎𝑛𝑐𝑒 𝑤𝑢𝑒ℎ 𝑎𝑚𝑎 𝑤𝑎𝑐ℎ𝑎 𝑡𝑢” Princess Esther.
Matara alitiwa mbaroni saa chache baada ya mwili wa Wahu kupatikana ukiwa unavuja damu ndani ya nyumba ya AirBnB mtaani South B.
Kwa sasa yuko chini ya ulinzi japo kuna idadi kubwa ya warembo wengine ambao wamejitokeza na kusema wamewahi pitia katika mikono yake ya ukatili na kunusurika kifo.
Starlet Wahu alizikwa Jumamosi alasiri Kamulu, viungani mwa jiji la Nairobi katika hafla iliyoharakishwa na kuhudhuriwa na watu wa familia pekee.