logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Stevo Simple Boy ndio msanii pekee ako juu ya KRG kwa sasa nchini Kenya - MP Jalang'oo

"Msanii pekee ambaye kwa sasa nchini Kenya yuko juu ya KRG ni Stevo Simple Boy peke yake"

image
na Davis Ojiambo

Burudani11 January 2024 - 07:42

Muhtasari


  • • Alimsifia Stevo Simple Boy akisema kuwa kwa sasa yeye hana mshindani. Mbunge huyo pia alidai kuwa amezikariri ngoma karibia zote za Stevo.
Jalang'oo amsifia Stevo kuwa juu ya KRG

Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor maarufu kama Jalang’oo amedai kwamba hakuna msanii ambaye yuko juu ya KRG kwa sasa nchini Kenya kimuziki isipokuwa rapa Stevo Simple Boy pekee.

Akizungumza jioni ya Jumatano kaitka hafla ya uzinduzi wa kolabo ya KRG na Konshens – Time Bomb, Jalang’o alimsifia KRG pakubwa akisema kuwa wengi wanadhani msanii huyo anayejitapa kuwa mkwasi hana talanta lakini ukweli ni kwamba talanta yake bado ni mbivu sana.

“Hiyo ngoma ni kali sana, nafikiri kwa muda mrefu KRG amekuwa akiwadanganya watu kuwa hana talanta lakini kwa hii ameifanyia haki. KRG amekuwa na talanta kutoka kitambo, yeye amepiga mashoo na kuimba ngoma kubwa kubwa,” Jalang’oo alisema.

“…Namuambia aendee hivyo venye yuko, na aendelee kusukuma. Msanii pekee ambaye kwa sasa nchini Kenya yuko juu ya KRG ni Stevo Simple Boy peke yake, hao wengine wako chini. Ni Stevo pekee ako juu ya KRG,” Jalang’oo aliongeza.

 Alimsifia Stevo Simple Boy akisema kuwa kwa sasa yeye hana mshindani. Mbunge huyo pia alidai kuwa amezikariri ngoma karibia zote za Stevo.

“Ninazijua ngoma zake [Stevo] kama zote. Huyo ni hatari. Unajua mimi nimekuwa shabiki wa Stevo kuanzia kitambo, tangu ‘vijana tuache mihadarati’ mpaka wakati alianza kuchumbiana Pritty Vishy mpaka juzi vile aliacha kumsalimia,” Jalang’oo alisema.

Kwa upande wake KRG akizungumzia Zaidi kuhusu kolabo hiyo na mkali kutoka Jamaika, alisema kuwa imemfungua mawazo ya kutaka kuchukulia muziki kwa umakini Zaidi muda wote kama biashara, jambo ambalo kwa muda mrefu hakuwa tayari kulifanya.

Pia alisema alijitolea pakubwa kufanikisha ubora wa ngoma kutoka kwa sauti hadi kwa video na kila kitu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved