• Msanii huyo alishangaa kama bili ya kiasi hicho chote cha pesa ni kwa nusu mwezi, vipi kuhusu bili ya mwezi mzima.
• “KPLC imenipa bili yangu ya Januari katikati ya mwezi na ni sh17k kubwa mno!!!! 🤦🏾♂️” Bien alistaajabu.
Msanii kiongozi wa bendi lililosambaratika la Sauti Sol, Bien Sol ameonyesha kutorishika kwake baada ya kampuni inayosimamia umeme nchini KPLC kumpa bili ndefu ya umeme kwa nusu mwezi.
Bien Baraza kupitia ukurasa wake wa X, awali ukijulikana kama Twitter, alionesha kukerwa kwake akisema kwamba alishangaa kupewa bili ya shilingi elfu 17 pesa za Kenya kama bili ya nusu mwezi.
Msanii huyo alishangaa kama bili ya kiasi hicho chote cha pesa ni kwa nusu mwezi, vipi kuhusu bili ya mwezi mzima.
“KPLC imenipa bili yangu ya Januari katikati ya mwezi na ni sh17k kubwa mno!!!! 🤦🏾♂️” Bien alistaajabu.
Itakumbukwa Bien si mtu maarufu wa kwanza kulalamikia bili za juu za umeme licha ya kwamba hawawezi kukumbuka kikubwa walichofanya kwa bili hiyo kufika kiwango hicho.
Mwezi Desemba mwaka jana, mtangazaji Anita Nderu naye alilalamika vikali baada ya KPLC kumpa bili ambayo alisema ilikuwa imechagizwa.
Akimtumia Insta Story Nderu alidai kuwa amelipa jumla ya Sh383,847 kama bili ya umeme kwa mwaka huo kufikia sasa.
Aliendelea kueleza kushtushwa kwake na ukweli akisema kiasi hicho ni kikubwa sana kuliko takwimu iliyotarajiwa.
Kulingana na Anita, bili yao ya umeme inapaswa kuwa kati ya Sh8,000 hadi Sh9,000.
"Nilipokagua bili mwezi huu nilishtuka!!! Tafadhali kumbuka hakuna kilichobadilika katika matumizi yetu mwaka mzima. Miezi ambayo hata hatuko nyumbani bili yetu ni kubwa kuliko miezi tuliyo nyumbani. Huduma ya wateja wa KPLC tafadhali fanya hii ina maana."
"Nilipouliza ulilaumu friji yetu, mfumuko wa bei, na dola. Hii ni."
Aliongeza:
"Na kwa namna fulani gari letu ambalo lina mita tofauti ambayo tunatoza kila siku limetugharimu chochote mwaka mzima? Tafadhali fanya jambo la maana. Kwa muktadha, bili yetu ilikuwa sh8,000-9,000 kwa mwezi."
Mnamo Agosti mwaka jana, KPLC ilikanusha madai kwamba ilitia chumvi bili za umeme za watumiaji kwa hadi asilimia 20 ya nishati ambayo haikutumiwa.