logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Obinna achukizwa na shabiki kumwambia kuwa anaishi kwa nyumba za kupanga

“Baba mzuri… anayetumia pesa vibaya kwa nyumba za kupanga,” shabiki huyo alimwandikia.

image
na Davis Ojiambo

Burudani19 February 2024 - 08:29

Muhtasari


  • • “Baba mzuri… anayetumia pesa vibaya kwa nyumba za kupanga,” shabiki huyo alimwandikia.

Mchekeshaji na YouTuber Oga Obinna amechukizwa baada ya kubaini kwamba kuendelea kuishi kwake katika nyumba za kupanga licha ya kuwa mmoja wa watu maarufu nchini kunawachukiza baadhi ya mashabiki wake.

Hii ni baada ya shabiki mmoja kwa jina Kenzy Kenzia Abba kuingia kwenye DM yake katika mtandao wa Instagram na kumpaka tope usoni akiwambia kwamba anaharibu pesa kwa kuendelea kuishi katika nyumba za kupanga.

Kwa mujibu wa shabiki huyo, Obinna anajifanya kuwa ni baba mzuri kwa watoto wake wanaoishi na babymamas wake kwa kuwapangia maisha mazuri katika nyumba za kupanga badala ya kujijengea kwake.

“Baba mzuri… anayetumia pesa vibaya kwa nyumba za kupanga,” shabiki huyo alimwandikia.

Obinna alichapisha ujumbe huo kutoka kwa huyo shabiki na kusema kwamba hakuwa anajua kwamba kuishi maisha yake kwa nyumba za kupanga kungewaudhi baadhi ya watu.

Kwa utani, alisema kwamba alikuwa sasa anapiga tathmini ya kuhama nyumba za kupanga ili kuishi katika nyumba yake ambayo amaijenga, japo kijijini mwao.

Wueh!! Wacha nitoke rentals niishi kwangu penye nimejenga ushago since kuna wale nawakosea sanaaaa🤣🤣🤣🙆🏿🙆🏿🙆🏿🙆🏿 Poleni Jamani sio kupenda kwangu.”

Huku mashabiki wake wengi wakimuunga mkono kwa kumkashifu mkosoaji huyo, wengine waliunga mkono hoja yake wakishikilia kuwa Obinna ni tajiri wa kutosha kumiliki nyumba na si kuishi kwa kupangisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved