logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilitumia 165K kwenye mavazi yangu katika date na Betty Kyallo - Stevo Simple Boy asema

“Gharama zote za Betty ni mimi niligharamia." Stevo alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani04 March 2024 - 06:18

Muhtasari


  • • Stevo alisema kwamba Betty Kyallo alipomuona kwenye muonekano wake wa kibabe kwa mara ya kwanza, alishtuka na kubabaika.
Kyallo na Stevo

Stevo Simple amefichua kwamba alitumia Zaidi ya laki moja na elfu 60 kwenye muonekano wake katika mtoko na mwanahabari Betty Kyallo.

Msanii huyo alikuwa anazungumza kwa mara ya kwanza kwenye mahojiano na mwanablogu Trudy Kitui ambapo alisema kwamba viatu pekee vilimgharimu elfu 40 pesa za Kenya.

 Kwa hesabu ya haraka haraka, Stevo alifichua kwamba nguo pekee zilichukua elfu 125, na kusema kwamba alitumia kiasi hicho chote cha pesa kutokana na mapenzi yake ya dhati kwa Kyallo.

“Mavazi yangu yalinigharimu pesa nyingi. Kwanza koti, suruali na tai vyote vilichukua 125,000. Viatu peke yake vilichukua 40,000. Kwa hiyo hesabu yote ilikuja kama 165,000,” Stevo alidadavua hisabati.

Stevo alisema kwamba Betty Kyallo alipomuona kwenye muonekano wake wa kibabe kwa mara ya kwanza, alishtuka na kubabaika.

“Betty kwamba alibabaika, aliniambia eeh Stevo kwani ulikuwa umenisubiria na haya mavazi yote. Nilivaa kwa ajili yake,” aliongeza.

 Lakini pia, msanii huyo alifunguka kwa undani sababu yake kuu kumpeleka Betty Kyallo kwenye dinner.

Alisema;

“Betty Kyallo nilikuwa nataka kumuonesha upendo wangu kwake. Ilikuwa ni mwanzo tu wa mapenzi yangu na tukiendelea basi atapata mapenzi ya dhati kutoka kwangu.”

“Tulipanga kwanza kukutana na familia zetu, kutoka hapo tupange harusi lakini aliniambia nimpe muda kidogo na atanipa jibu. Betty alinifurahisha kwa kuongea, ako tu sawa. Yeye ni mcheshi na mimi ni mcheshi kwa hiyo tuliendana.”

“Gharama zote za Betty ni mimi niligharamia. Na ikitokea amenikubalia, nitampa mapenzi ya dhati, nitamuelewa naye pia anielewe, tufanye kazi pamoja, tushirikiane. Mambo yake ni yangu na yangu yatakuwa yake,” alimaliza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved