Ruth K ampa kama zawadi Dem wa FB nguo zake alizokuwa akivaa kabla ya ujauzito

Ruth K kwa upande wake alisema bado ako na nguo nyingi ambazo hazimtoshi kwa sasa na kufichua kwamba ana mpango wa kugawa angalau nguo kati ya 3-5 kama zawadi kwa shabiki wake mmoja.

Muhtasari

• "Nawaambianga kila siku mkuwe na hawa mabeshte wameomoka," Dem Wa Facebook alisema huku akisubiri kwa furaha Ruth K ampe nguo zaidi.

Ruth K na Dem wa FB.
Ruth K na Dem wa FB.
Image: Screengrab

YouTuber Ruth K ambaye pia ni mpenzi wa mchekeshaji Mulamwah amempa kama zawadi mchekeshaji chipukizi Dem wa FB baadhi ya nguo zake ambazo alikuwa anavaa kabla ya kupata ujauzito.

Katika video ambayo alipakia kwenye jukwaa lake la YouTube, Ruth K alitembelewa na Dem wa FB katika makazi yao mapya.

Kama kawaida yake, Dem wa FB alikuwa anawatania kwa mada mbali mbali kutoka kwa makazi ya kifahari walimohamia wiki chache zilizopita hadi kwa gari la kifahari aina ya Mercedes ambalo walinunua wiki jana.

Baadae walimkaribisha ndani ya nyumba yao na alipoketi kwenye sebule, Ruth K aliinia chumbani na kurudi na rundo la nguo zake alizosema zimekuwa ndogo kwake baada ya kujifungua.

"Nikijaribu kuvaa na chini ama juu haipiti. Wacha nipee Dem Wa Facebook halafu zenye zitabaki tuone vile tutafanya," Ruth K alisema.

Akimsifia, Dem wa FB alisema kwamba wamejuana na Ruth K kwa muda mrefu, tangu enzi wakiwa shule ya upili pamoja.

“Akon a roho nzuri sana, tumejuana tangu shule ya upili, si eti nakusifia bure, si rahisi upate marafiki walianza kusoma shule moja wanapendana, Zaidi ya miaka 10 huku nje bado wanapendana, san asana warembo ni ngumu sana,” Dem wa FB alisema.

Dem wa FB alizipokea nguo hizo kwa bashasha na kusema aongezewe zingine hadi zifike nguo 20, awamu ya kwanza waliehesabu zenye alipew zikafika 7.

"Nawaambianga kila siku mkuwe na hawa mabeshte wameomoka," Dem Wa Facebook alisema huku akisubiri kwa furaha Ruth K ampe nguo zaidi.

Dem wa FB alisema kwa furaha kwamba angalau amepata nguo nzuri za kuvaa kwenda kanisani, akisema kwamba Jumapili hii kwa mara ya kwanza mwaka huu ataingia kanisani baada ya kupata nguo nzuri kutoka kwa rafiki wake wa shule ya upili.

Ruth K kwa upande wake alisema bado ako na nguo nyingi ambazo hazimtoshi kwa sasa na kufichua kwamba ana mpango wa kugawa angalau nguo kati ya 3-5 kama zawadi kwa shabiki wake mmoja.