YouTuber Nicolas Kioko amefunguka jinsi mtandao huo wa video unavyolipa watumizi wake, haswa kutoka humu nchini.
Kioko ambaye anasema yeye hutumia YouTube kama sehemu yake ya kupata riziki alisema katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha redio humu nchini kwamba jinsi ambavyo YouTube inawalipa watu wa humu nchini si sawa na jinsi inavyowalipa walioko kwenye mataifa ya nje, haswa Marekani.
Alifichua kwamba nchini Kenya, kwa kila watazamaji milioni moja kwenye video yako, YouTuber analipwa kati ya kiasi cha elfu 80 hadi laki moja, kinyume na Marekani ambapo kwa watazamaji sawa na hao, YouTuber analipwa hadi dola elfu kumi.
“Kufanya content creation ni ghali hata kama inalipa lakini si sana. Ni vile zile views mimi Napata hapa Kenya, kawaida mimi Napata wastani wa 2.5m views hadi 3.5m views. Nikiwa na hizo views nikiwa USA mimi nakaa kama rais, lakini hapa ukiwa na 1m views unapata tu kati ya 80-100k, lakini ukiwa USA utapata kama Ksh. 1.3M,” Kioko alisema.
Baba huyo wa mapacha alisema kwamba ni kazi ngumu kwa content creators nchini kuendelea kwa kile alisema kwamba YouTube hailipi vizuri kwa YouTubers wa humu nchini.
Alikubaliana na maoni ya awali ya TikToker Sammy Kioko kwamba tangu aingie kwenye kukuza maudhui, ameenda hasara ya Zaidi ya shilingi milioni 2.
Kioko pia alisema kwamba kushuka kwa sarafu ya Euro pia kunawaathiri content creators wa humu nchini.