Obinna aweka wazi uhusiano wake halisi na Dem wa Facebook

“Dem Wa Facebook sio type yangu! Hawezi kamwe kuwa aina yangu!," alisema.

Muhtasari

•Nina nia njema na Dem Wa Facebook; yeye anajua, wazazi wake wanajua, usimamizi wangu unajua, management yake inajua, period," alisema.

•Obinna anaendelea kushikilia uamuzi wake kwamba hatamuoa Dem Wa Facebook kwa sababu yeye si type yake na hatawahi.

OGA OBINNA
Image: KWA HISANI

Mchekeshaji Obinna amefafanua uhusiano wake na Dem Wa Facebook.

Akizungumza na waandishi wa habari katika onyesho la kwanza la filamu ya King Kaka ya Monkey Business, Obinna alisema kuwa anamuweka karibu Dem Wa Facebook kwa sababu ana nia nzuri naye, na hakuna kingine zaidi yake.

“Nitakachosema ni hiki: Chochote ninachofanya na kuchagua kusema ni juu yangu kabisa; hata hivyo unaelewa au kutafsiri, ni juu yako kabisa, na sio jambo langu!

Nina nia njema na Dem Wa Facebook; yeye anajua, wazazi wake wanajua, usimamizi wangu unajua, management yake inajua, period! Hata hivyo, ukisoma, ni juu yako.” Obinna alisema.

Obinna alisema kuwa yeye hajali kile ambacho umma unafikiri kwani anataka tu kilicho bora kwa Dem Wa Facebook, na hajali nini kinaweza kutokea baadaye anachotaka ni kuona kuwa amemsaidia akuwe  bora Zaidi.

"Ninaweza kufanya chochote ninachofanya baada ya miaka miwili na baadaye anigeuke. Lakini tunasamehe na kusahau lakini sitawacha kufanya wema,” Obinna aliongezea.

Obinna anaendelea kushikilia uamuzi wake kwamba hatamuoa Dem Wa Facebook kwa sababu yeye si type yake na hatawahi.

“Dem Wa Facebook sio type yangu! Hawezi kamwe kuwa aina yangu!.

 Mumemwona yuko na talanta na pia yuko na heshima sana.Katika miaka 5 ijayo, atakuwa tofauti kabisa kwa sababu ya mipango niliyo nayo kwa ajili yake,” Obinna aliongezea.