Tiktoker Kelvin Kinuthia alishindwa kuzuia furaha yake baada ya wanafamilia wake kujumuika pamoja na kumfanyia bonge lla surprise.
TikToker huyo alichukua katika ukurasa wake wa Instagram kuonyesha kionjo cha video jinsi mamake na dadake walimkabidhi zawadi hio iliyokuwa imefichwa ndani ya shada la maua.
Baada ya kuichomoa, alipigwa na butwaa kupata ni simu aina ya iPhone 15 pro max yenye uwezo wa kubeba video na nyimbo kwa hadi 1TB.
Kinuthia alishindwa kuzuia machozi yake ya furaha na kusema kwamba zawadi ya simu ya iPhone 5 ndicho kitu ambacho amekuwa akililia ngoa kwa muda mrefu.
“Weeh guys lemme tell you my family did it ❤️Aki waah hata nakosa maneno❤️ Dada yangu na mama yangu walinishangaza kwa zawadi yangu ya ndoto❤️❤️Am such a proud girl kuwa na wanafamilia kama hao ❤️Asante Mama, Asante Maureen ,Asante zaituni,” Kinuthia alisema, akijisisitizia kuwa yeye ni msichana.
“Weeh Leo ni Leo 😩❤️Mwishowe nilipata hisia ya mshangao 😩❤️Familia yangu ilifanya muujiza. MTUMIAJI mpya kabisa wa iPhone 15 pro max 1TB mwaka wa 254❤️ Asante kwa mama na dada yangu kwa mshangao huu mzuri na mzuri ❤️Nina furaha sana hata sina maneno ya kuelezea au kuelezea furaha yangu,” aliongeza.