logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Brenda Jons aelezea sababu za mapumziko katika mitandao ya kijamii

Nilichukua miezi 3 ya mapumziko katika mitandao ya kijamii ili kuzama na kumsikia Mungu kwa ufasaha zaidi

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 May 2024 - 08:38

Muhtasari


  • •"Nilichukua miezi 3 ya mapumziko katika mitandao ya kijamii ili kuzama na kumsikia Mungu kwa ufasaha zaidi. Imekuwa likizo nzuri zaidi kuwahi kutokea." Brenda Jons alisema.
  • •Jons alikiri kwamba kwa kipindi kikubwa, alikuwa ameruhusu mitandao ya kijamii kufafanua utambulisho wake

Mtayarishaji wa maudhui nchini Kenya Brenda Jons amerejea tena katika mitandao ya kijamii akitaja upya wa kiroho kuwa sababu iliyomfanya kuchukua mapumziko katika mitandao ya kijamii.

Katika chapisho la hivi majuzi kwenye mitandao ya kijamii, mtayarishaji wa maudhui alifichua kwamba alikuwa amechukua mapumziko ya miezi mitatu ili kuimarisha uhusiano wake na imani yake.

"Nilichukua miezi 3 ya mapumziko katika mitandao ya kijamii ili kuzama na kumsikia Mungu kwa ufasaha zaidi. Imekuwa likizo nzuri zaidi kuwahi kutokea." Brenda Jons alisema.

Jons alikiri kwamba kwa kipindi kikubwa, alikuwa ameruhusu mitandao ya kijamii kufafanua utambulisho wake, lakini aliona ni wakati wa kujitambua upya na imani yake akinukuu mstari kutoka kwa Biblia.

“Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, kabla hujazaliwa nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa,” akasema.

"Nilihitaji kujua mtu huyo ni nani. Ananifafanuaje na ni Mungu gani mwaminifu."

Wakati wa mapumziko, Brenda Jons alishiriki kwamba alijitolea kusoma Biblia kwa bidii zaidi, akiruhusu mafundisho ya Biblia kumuongoza.

Aliangazia umuhimu wa kutafakari na akataja mstari wa Injili kulingana na Yohana.

 "Kondoo huitambua sauti ya mchungaji, yeye anayewalisha, kuwaongoza, na kuwalinda Sasa ninaweza kumsikia zaidi. Jinsi nzuri," alisema.

"Nimewakumbuka marafiki, Bwana amekuwa akikufundisha nini?" Aliuliza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved