logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kabugi atangaza kujiingiza kujitosa kwenye siasa 2027

Hata hivyo, hakutaja kama angekuwa mgombea binafsi au kama angejiunga na chama cha siasa.

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 May 2024 - 11:30

Muhtasari


  • •Kwenye mahojiano na Oga Obinna,Kabugi ameweka nia ya kujiingiza kwenye siasa 2027 kuwania nafasi ya ubunge au useneta kaunti ya Nakuru.
  • •Hata hivyo, hakutaja kama angekuwa mgombea binafsi au kama angejiunga na chama cha siasa.
Picha:Instagram

 Kennedy Kabugi,mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali,alitangaza nia yake ya kujiunga na siasa za kitaifa mnamo Jumatatu, Mei 27, 2024

Kwenye mazungumzo na Oga Obinna, Kabugi alithibitisha kuwa jina lake litakuwa kwenye karatasi ya kura katika uchaguzi mkuu wa 2027.

'2027 nitashiriki kwenye kura ...' Kabugi alisema

Kabugi aliiwahakikishia watu kutoka mji aliozaliwa, eneo bunge la Nakuru Mashariki, kijana huyo mbunifu alisema kwamba atajaribu kugombea kiti cha ubunge, na ikiwa mambo hayataenda kama alivyopanga basi atajaribu nafasi ya juu zaidi kama Seneta lakini hatathubutu kuwania nafasi ya Gavana.

'Nitajaribu Ubunge ikiwa mambo hayaendi kama nilivyopanga nitagombea useneta lakini sitajaribu wadhifa wa ugavana," alisema. Hata hivyo, hakutaja kama angekuwa mgombea binafsi au kama angejiunga na chama cha siasa.

Tumekuwa tukishuhudia watu mashuhuri wengi wa Kenya  wakiwemo wanahabari, waigizaji, , wanamuziki,  na waundaji wa maudhui wakibadilisha  taaluma zao na kujiingiza kwenye siasa.Huku wengine wakifaulu na wengine kupoteza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved