logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ezekiel Mutua anasherehekea mapato yake ya kwanza kutoka kwa TikTok

Natumai kuwa mfano kwamba si lazima maudhui yawe machafu ili kuuza

image
na Davis Ojiambo

Burudani29 May 2024 - 08:23

Muhtasari


  • •Ezekiel Mutua alionyesha furaha yake baada ya kupata  Pesa kwa mara ya kwanza kutoka TikTok.
  • •Kauli ya Mutua sambamba na picha hiyo ilitangaza kuanza kwa misheni yake ya kusafisha jukwaa hilo na kuwa na maudhui ya maana haswa yanayolenga vijana.
Ezekiel Mutua

Mkurugenzi ya Chama cha Hakimiliki ya Muziki Kenya (MCSK) Ezekiel Mutua amesherehekea mapato yake ya kwanza kutoka kwa TikTok.

Mtetezi wa maudhui safi alishiriki msisimko wake hadharani.

Katika mtandao wake wa kijamii, alichapisha picha inayoonyesha kiwango cha  KSh 1,374 kutoka TikTok hadi akaunti yake ya PayPal.

Kauli ya Mutua sambamba na picha hiyo ilitangaza kuanza kwa misheni yake ya kusafisha jukwaa hilo kwa maudhui  yanayofaa, haswa kwa vijana.

Alionyesha kujitolea kwake kuthibitisha kwamba mtu anaweza kufaulu kwenye TikTok na maudhui ya heshima.

“Saa 10:20 jioni leo, nilitoa pesa yangu ya kwanza kutoka kwa TikTok kupitia akaunti yangu ya PayPal. Safari ya kutakasa TikTok kupitia maudhui safi imeanza kwa dhati.

Natumai kuwa mfano kwamba si lazima maudhui yawe machafu ili kuuza," aliandika.

Mkurugenzi huyo aliongezea kuwa ni hamu yake ya kupata pesa nyingi zaidi kwenye jukwaa hilo kupitia maudhui safi.

"Siku moja, nitachapisha milioni moja hapa kupitia maudhui safi na muhimu kwenye TikTok." aliandika.

Haya yanajiri takriban wiki moja baada ya kufanya mkutano na mhubiri mwenye utata Victor Kanyari kuhusu mwenendo wake jukwaani katika wiki chache zilizopita.

Ezekiel Mutua alikashifu tabia yake akisema alikuwa akionyesha mfano mbaya kwa vijana kwenye TikTok na wafuasi wake kwa vile ana kanisa.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved