Dj shiti azungumzia umuhimu wa kujitegemea kifedha

“Hakuna kitu mbaya kama kuomba omba,Kukuwa na pesa yako fulani ni kitu fiti sana" alisema.

Muhtasari

•Dj Shiti alizungumzia umuhimu wa kuwa na pesa zako binafsi, sio tu kama mwanaume bali pia mtu yeyeto, akisema inakupa heshima kutoka kwa wengine.

•Alisema hali mbaya zaidi ambayo hupaswi kamwe kujikuta ni kuwa umekosa pesa kwa sababu siku zote watu wanatumia hilo kujinufaisha na kukushusha hadhi.

dj-shiti
dj-shiti
Image: instagram

Mchekeshaji kutoka nchini Kenya DJ Shiti amezungumzia umuhimu wa kujitegemea kifedha hasa wanaume.

Dj Shiti alizungumzia umuhimu wa kuwa na pesa zako binafsi, sio tu kama mwanaume bali pia mtu yeyeto, akisema inakupa heshima kutoka kwa wengine.

“Kukuwa na pesa yako fulani ni kitu fiti sana hizo za free zinaisha kwa machozi. Hiyo hata niliona the time niko na buda hosi last year niliona nikarealize kua na dooh yako ni poa.” DJ Shiti alieleza.

DJ Shiti, ambaye alikuwa akisimulia jinsi alivyokuwa akikabiliana na ugumu wa Maisha.

Alisema hali mbaya zaidi ambayo hupaswi kamwe kujikuta ni kuwa umekosa pesa kwa sababu siku zote watu wanatumia hilo kujinufaisha kwa kukushusha hadhi.

 Wakati  watu washa jua mambo yako sio sawa watu hukutreat tuh vibaya.

Ni poa ukiwa na pesa fulani nilikua na mzae hosy last year nilikaa huko sana mpaka hakuna product nilikua na endorse mpaka kidogo pesa yangu iishe.

Watu wanakubeba ndogo sana, ukiwa na pesa yako na unaweza lipa nyumba ukule breakfast, lunch na supper ni kitu fiti sana…hakuna kitu mbaya kama kuomba omba," Dj shiti alisema.

Aliendelea kueleza jinsi pesa pia ni kitu muhimu katika mahusiano, akisema kuwa na pesa, hata hiwe kidogo.

Alieleza kuwa itasaidia kudumisha uhusiano wako kwa sababu utahitaji chakula cha kula, pamoja na mambo mengine muhimu.

“Same ina apply kwa dem, kwa sababu watahitaji mambo ya msingi tu, kama huna pesa haitapendeza kabisaa,” DJ Shiti alisema.