Baba aonyesha meseji kutoka kwa mwanawe wa kambo akimuonya dhidi ya kujaribu kumuadhibu

Kilichomchanganya zaidi ni kwamba baada ya kuonyesha mamake mtoto ujumbe,alisema mtoto yuko sahihi kumtaka asimchape kwani jukumu lake linaishia katika kumlea tu kama baba wa kambo na si kumfunza adabu.

Muhtasari

• “Mimi sio mwanao, usidhubutu hata kuniadhibu,” ujumbe huo kutoka kwa yule aliyedai ni mwanawe wa kambo ulisoma.

Image: BBC

Mwanamume mmoja raia wa Afrika Kusini amewashangaza wengi katika jukwaa la X – zamani likijulikana kama Twitter – baada ya kuonyesha ujumbe wa vitisho na masharti makali kutoka kwa mwanawe wa kambo.

Mtu huyo kwa jina la Dr Shiyakilenga alituma picha ya mazungumzo kwenye mtandao wa WhatsApp na mtu aliyedai ni mwanawe wa kambo.

Alisema kwamba alishangazwa kupokea ujumbe huo, mwanawe wa kambo alimpa onyo kali dhidi ya kujaribu kumuadhibu hata kidogo kwani yeye ni mwanawe.

“Mimi sio mwanao, usidhubutu hata kuniadhibu,” ujumbe huo kutoka kwa yule aliyedai ni mwanawe wa kambo ulisoma.

Dr Shiyakilenga alisema kwamba ujumbe huo wa onyo kutoka kwa mtoto aliyekubali kumlea kama mwanawe wa kumzaa baada ya kuoa mamake ulimuacha na mshtuko mkubwa, akishindwa cha kufanya.

Kilichomchanganya Zaidi ni kwamba baada ya kuonyesha mamake mtoto, ambaye ni mke wake ujumbe ule, mama alisema kwamba mtoto yuko sahihi kumtaka asimchape kwani jukumu lake linaishia katika kumlea tu kama baba wa kambo na si kumfunza adabu.

“Mwanangu wa kambo alinitumia maandishi haya, nikamuonyesha mama yake na akasema yuko sawa. Nilijaribu kupiga hatua ikanigukia. Nimeshajitoa,” alisema.

Je, ni sahihi kwa baba kumfunza adabu mtoto wake wa kambo?

Tazama chapisho hili hapa kisha utoe maoni yako