Claudia Naisabwa apuuza uhusiano na Rayvanny akisema ni marafiki tu

“Rayvanny na mimi ni marafiki. Ni kweli kabisa kwamba tuna mahusiano ya kikazi,” alisema.

Muhtasari

•Claudia amejikuta akihusishwa na baadhi ya majina makubwa kama Rayvanny ambao watu walidhani wako katika mahusiano naye.

•Aliongezea kuwa hayuko kwenye mahusiano yoyote akisema kwa sasa mtazamo wake ni kujitafutia maisha bora kwanza.

Claudia Naisabwa
Image: Instagram

Claudia Naisabwa amejipatia umaarufu kama Gen Z MCee bora akiwa na umri mdogo sana.

Hili halijamfungulia milango tu bali limemwezesha kukaa meza moja na watu mashuhuri na hivyo kumkuza zaidi.

Pamoja na hayo, pia amejikuta akihusishwa na baadhi ya majina makubwa kama Rayvanny ambao watu walidhani wako katika mahusiano naye.

Hata hivyo akiongea na Mungai Eve kwenye mahojiano ya hivi majuzi, kwa mara ya kwanza alifunguka kuhusu madai yake ya uhusiano na Rayvanny akisema walikuwa marafiki tu.

“Rayvanny na mimi ni marafiki. Ni kweli kabisa kwamba tuna mahusiano ya kikazi, kwa hivyo watu wanaweza kutafsiri hivyo vibaya,” alisema.

Claudia aliendelea kufichua kuwa kujihusisha kwake na mwimbaji huyo wa Kiswahili haikuwa chochote ila biashara.

“Hakuna zaidi. Sisemi kwa njia mbaya Sisi ni waburudishaji hivi ndivyo tunavyojitafutia riziki. Unapomwona mwigizaji akimbusu mtu,utasema wako kwa mahusiano? Hiyo ndiyo asili ya kazi yao,” aliongezea.

Aliongezea kuwa hayuko kwenye mahusiano yoyote akisema kwa sasa mtazamo wake ni kujitafutia maisha ya bora kwanza.

“Mimi siko katika uhusiano, na sina nia ya kuingia kwenye uhusiano wowote kwa sasa.

Mtazamo wangu uko kwangu na mimi peke yangu kwa muda mrefu.

Inasikitisha sana kwamba kila wanapomwona mwanamke mchanga aliyefanikiwa, wanataka kumuoanisha na mtu Fulani,”alisema.