Kennedy Rapudo aeleza jinsi alivyopata na Amber Ray

“Mimi ndiye nilienda huko na kuongea naye, nikikiri kwamba alikuwa mrembo, na nilikuwa nimemuona kwenye mitandao ya kijamii."

Muhtasari

•Rapudo alieleza kwa nini hakupoteza muda wake alipogundua Amber Ray alikuwa single akisema ni kwa sababu alikuwa kwenye foleni akingoja karibu miaka 2.

•Rapundo alieleza kuwa alichukua hatua ya kwanza ya kumsogelea na kuanza mazungumzo ya kumfahamu Amber Ray.

Kennedy Rapudo na mkewe Amber Ray
Kennedy Rapudo na mkewe Amber Ray
Image: Instagram

Mfanyabiashara Mkenya Kennedy Rapudo  amefichua jinsi alivyokutana na sosholaiti Mkenya Amber Ray, ambaye sasa ni mama wa watoto wake.

Akiongea kwenye mahojiano mafupi na Parents Magazine, Rapudo alifunguka na kusema kuwa  alikutana na Amber Ray kwenye ukumbi wa outdoor park and chill.

“Alinikatia, kulikuwa mahali huko Thika road, ambapo watu walienda kuegesha magari, kutuliza, na kunywa.

 Kwa hivyo, nilienda pale nikiwa nimeegesha gari, na ndipo nikagundua kuwa kuna mwanamke ambaye alikuwa akinitazama kwa namna fulani iliyonifanya nitamani kumkaribia.”

Anaendelea kueleza kuwa alichukua hatua ya kwanza ya kumsogelea na kuanza mazungumzo ya kumfahamu.

Walikutana tena, na mara wakaachana na wapenzi wao, wakaanza kuchumbiana.

“Mimi ndiye nilienda huko na kuongea naye, nikikiri kwamba alikuwa mrembo, na nilikuwa nimemuona kwenye mitandao ya kijamii.

Alikua na mtu na mimi nilikua na mtu, the moment alikua single hivi nikaingia mbio.” Kennedy Rapudo alisema.

Rapudo alieleza kwa nini hakupoteza muda wake alipogundua Amber Ray alikuwa single , akisema ni kwa sababu alikuwa kwenye foleni kwa karibu miaka 2.

Zaidi ya hayo, ilikuwa rahisi kumshinda kwa sababu tayari alikuwa ameshajenga hamu ya kuwa naye, jambo ambalo lilikubalika.

“Kwa kweli alikuwa akijaribu kuniunganisha na rafiki yake mmoja, lakini nilipendezwa naye, kwa hivyo siku moja, aliniuliza ikiwa tunaweza kunywa glass of wine, na iliyobaki ni historia.” Kennedy alieleza.