Wapenzi wa zamani wa Diamond, Hamisa na Wema sasa watoshana kwa idadi ya followers Instagram

Itakumbukwa kwamba kinachowavutia wengi ni ukweli kwamba wawili hao waliwahi kuwa wapenzi wa msanii mkubwa nchini humo, Diamond Platnumz ambaye pia ndiye mtu wa pekee kutoka Tanzania mwenye wafuasi wengi, Zaidi ya milioni 17.

Muhtasari

• Diamond mwanzo alichumbiana na Wema Sepetu kabla ya kuachana na baadae akachumbiana na Hamisa Mobetto.

Wema na Hamisa
Wema na Hamisa

Hamisa Mobetto sasa amemfikia mwenzake Wema Sepetu katika idadi ya wafuasi kwenye mtandao wa Instagram.

Kwa muda mrefu, Wema Sepetu  amekuwa mtumizi wa Instagram kutoka nchini Tanzania mwenye wafuasi wengi katika mtandao huo akiwa na wafuasi milioni 11.5.

Hamisa Mobetto sasa amekuwa wa pili kufikisha idadi hiyo ya wafuasi milioni 11.5.

Itakumbukwa kwamba kinachowavutia wengi ni ukweli kwamba wawili hao waliwahi kuwa wapenzi wa msanii mkubwa nchini humo, Diamond Platnumz ambaye pia ndiye mtu wa pekee kutoka Tanzania mwenye wafuasi wengi, Zaidi ya milioni 17.

Diamond mwanzo alichumbiana na Wema Sepetu kabla ya kuachana na baadae akachumbiana na Hamisa Mobetto ambaye walipata mtoto pamoja, mtoto ambaye amekuja kuibuka kuwa wa kuvutia mambo mengi mitandaoni wengi wakihoji uhalali wa Diamond kuwa babake wa kumzaa.