Kakake Eric Omondi, Fred Omondi kuzikwa Juni 29 nyumbani kwao Sega, kaunti ya Siaya

Ken Waudo, mwenyekiti wa kamati inayoandaa mipango ya mazishi jijini Nairobi ametoa ratiba kwamba leo Alhamisi kutakuwa na ibada ya Wafu kwa ajili ya marehemu Fred Omondi katika kanisa la CITAM Valley Road kuanzia saa tano asubuhi.

Muhtasari

• Aidha, ratiba hiyo ilidokeza kuwa Ijumaa hii kutakuwa na tamasha kubwa la uchekeshaji litakaloandaliwa jijini Nairobi kwa ajili ya kumpa Fred heshima za mwisho.

Image: INSTAGRAM// FRED OMONDI

Kamati andalizi ya mipango ya safari ya mwisho duniani ya marehemu Fred Omondi imetoa rasmi ratiba ya mazishi ya mchekeshaji huyo ambaye alifariki Jumamosi iliyopita.

Fred Omondi, ambaye ni mdogo wake mchekeshaji aliyegeuka na kuwa mwanaharakati Eric Omondi alifariki Jumamosi alfajiri katika ajali ya barabara.

Ken Waudo, mwenyekiti wa kamati inayoandaa mipango ya mazishi jijini Nairobi ametoa ratiba kwamba leo Alhamisi kutakuwa na ibada ya Wafu kwa ajili ya marehemu Fred Omondi katika kanisa la CITAM Valley Road kuanzia saa tano asubuhi.

“Kufuatia kufariki kwa mwenzetu na mburudishaji Fred Odhiambo Omondi, almaarufu anayejulikana kama Fred Omondi, akiwa amelazwa katika chumba cha kuhifadhi maiti jijini Nairobi, kamati iko, kujiandaa na send-off yake ya mwisho kama ifuatavyo; Tutakuwa na Ibada ya ukumbusho wake jijini Nairobi katika Kanisa la CITAM kwenye Barabara ya Valley, Alhamisi tarehe 27 Juni 2024 kutoka 11:00 asubuhi,” sehemu ya ratiba hiyo ilisema.

Aidha, ratiba hiyo ilidokeza kuwa Ijumaa hii kutakuwa na tamasha kubwa la uchekeshaji litakaloandaliwa jijini Nairobi kwa ajili ya kumpa Fred heshima za mwisho huku tamasha sawia likiandaliwa katika klabu moja jijini Kisumu Jumamosi baada ya maziko.

“Kutakuwa na show ya kuchangisha fedha Fred Omondi; Kicheko cha Mwisho kwa Mgahawa wa Carnivore Simba Salon siku ya Ijumaa tarehe 21 Juni 2024 kuanzia saa 6:00 jioni, tunaomba wanachama wa umma kujitokeza kwa wingi kuunga mkono hoja. Utiaji saini wa kitabu cha maombolezo pia kutokea hapa. Mjini Kisumu, Da Place pia wamejitolea kuandaa ngoma ya mwisho ya Fred Omondi, hii itatokea Jumamosi tarehe 29 jioni.”