Babu Owino aeleza licha ya kuwa na Shughuli nyingi, analala nyumbani kila siku

Alisema kuwa mwanamume akimheshimu mke wake na pia kumtimizia mahitaji yake chumbani huimarisha ndoa.

Muhtasari

•Babu Owino aliorodhesha mambo anayofanya ili kuhakikisha ndoa yake inafanya kazi huku akiwashauri wanaume wafuate mfano wake.

•Pia aliongeza kuwa licha ya kuwa na shughuli nyingi, anahakikisha kuwa analala nyumbani na kumheshimu mke wake wakati wote.

Babu Owino na Mkewe
Image: Instagram

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amefunguka kuhusu jinsi anavyofanikisha ndoa yake licha ya majukumu yake mengi.

Mwanasiasa huyo mahiri alieleza kuwa licha ya kuwa mwanamume mwenye shughuli nyingi, anahakikisha analala nyumbani na kutenga muda kwa mkewe na familia.

Katika mahojiano na Oga Obinna, Babu alieleza kwamba ndoa ni taasisi rahisi, lakini watu wanapenda kufanya mambo kuwa magumu.

Hakika napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa mke wa ajabu. Mrembo wa kimwili, na mrembo moyoni.

 Mke mwenye furaha, maisha ya furaha. Baadhi ya watu wanasema ndoa ni utapeli lakini hawajui ni kitu gani, hawajui wafanye nini ndani ya ndoa,” alisema Babu.

Aliongeza kuwa ndoa inakuwa rahisi pale wapenzi wanapoelewana na watoto wao.

Pia alishiriki kuwa wanawake ndio watu rahisi kuwaelewa na akatoa vidokezo kwa wanaume jinsi ya kusimamia uhusiano.

 "Wanawake ndio wepesi wa kujifunza. Wathamini tu, na pili, wape muda.

Tumia wakati mzuri nao. Tatu, wasiliana nao kikamilifu. 

Wachukue wapeleke mahali fulani, haijalishi ni wapi, kiini ni kutumia wakati pamoja, "alisema.

Kulingana na Babu, ndoa yake si kamilifu, lakini amemwelewa mke wake, na anamuelewa kikamilifu.

Aliongeza kuwa mwanamume akimheshimu mke wake na pia kumtimizia mahitaji yake chumbani huimarisha ndoa.

Babu pia alijadili jinsi wanandoa wanapaswa kutatua masuala na kusimamia fedha na kushiriki jinsi vipengele hivyo viwili ni muhimu.

"Nina shughuli nyingi lakini nalala nyumbani na huwezi kuwa na shughuli nyingi kwa jambo muhimu au mtu muhimu maishani mwako.” Alisema.