Kando na ‘nyash’ nampenda sana Poshy Queen na tunafikiria kupata watoto - Harmonize

"Sisi huzungumza kuhusu maisha, ufanisi – tunataka sana kuwa matajiri, hivyo ninaweza sema kwamba ni kama mke wangu tu, kando na nyash na vitu vingine,” aliongeza.

Muhtasari

• Alimsifia mrembo huyo akisema katika kipindi cha miezi 6 ambayo wamekaa pamoja, ameona mabadiliko mengi katika maisha yake ikiwemo ufanisi maradufu kimuziki.

Harmonize na barafu ya moyo wake, Poshy Queen.
Harmonize na barafu ya moyo wake, Poshy Queen.
Image: Instagram

Harmonize amekiri kwamba hana mpango wowote wa kumchezea mpenzi wake mpya, Poshy Queen kwa kumtumia kimapenzi na kisha kumuacha baadae, akikariri msimamo wake kuwa anataka kutulia na kuanzisha familia.

Msanii huyo ambaye miezi michache iliyopita alisherehekea kufikisha umri wa miaka 30 alisema kwamba kwa sasa ashakuwa mtu mzima aliyekomaa kifikira na kimawazo na lengo lake ni zuri tu kwa Poshy Queen.

Aliradidi kwamba licha ya wengi kudai alimfuata Poshy Queen kutokana na umbile lake la kuvutia lenye kiuno pana, japo ni kweli lakini pia anampenda kwa dhati na wanafikiria kupata watoto miaka si mingi ijayo.

Alimsifia mrembo huyo akisema katika kipindi cha miezi 6 ambayo wamekaa pamoja, ameona mabadiliko mengi katika maisha yake ikiwemo ufanisi maradufu kimuziki.

“Nikiwa mkweli kabisa na kila mtu, ninakuwa na ujasiri mkubwa sana kumuambia mtu yeyote yule kwamba nampenda sana Poshy Queen. Na hili nalizungumza kando na kuwa na ile furaha, lakini unajua tumekuwa pamoja kwa Zaidi ya miezi 6 sasa.”

“Kando na nyash na kila kitu, ninampenda sana kwa vile amekuja na kubadilisha maisha yangu kwa ujumla, mimi ni mtu mpya sasa hivi, nafikiria kuhusu watoto, msukumo wa mafanikio umekuwa juhudi zake na hata huo mradi ambao niliufanya ni yeye alikuja na wazo hilo kunishauri nitengeneze albamu kumhusu rais,” Harmonize alisema.

“Kwa sasa tushatoka huko kwa maongezi ya nyash, sisi ni marafiki, tunazungumza kuhusu maisha ya baadae, kuhusu watoto na wakati mwingine tunajivinjari tunatoka tunafurahia glasi ya divai na Zaidi sisi huzungumza kuhusu maisha, ufanisi – tunataka sana kuwa matajiri, hivyo ninaweza sema kwamba ni kama mke wangu tu, kando na nyash na vitu vingine,” aliongeza.

Harmonize katika siku za hivi karibuni amekuwa akipunguza kumzungumzia mpenziwe mtandaoni, na huu uhusiano ulikuja takribani mwaka mmoja baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda, Frida Kajala Masanja.