Vanessa Mdee afanikiwa kufanya upasuaji wa jicho

"Upasuaji wako wa jicho ukifaulu, Utukufu kwa Mungu," alisema.

Muhtasari

•Vanessa Mdee alitumia fursa hio kumshukuru Mungu kwa kumsaidia katika hali yake.

•Pia aliwashauri watu kuongea na Mungu badala ya kuongea sana kila wakati wanapokuwa kwenye matatizo.

Vanessa Mdee
Image: Instagram

Mwimbaji wa Tanzania Vanessa Mdee alitumia kurasa zake za mitandao yake ya kijamii kuchapisha habari za upasuaji wake wa macho uliofanikiwa nchini Marekani.

 Alichapisha video akicheza na mumewe Rotimi, wote wakiwa katika hali nzuri, huku Mdee akiwa na kifaa kilicho funika  jicho alilofanyiwa upasuaji.

"Upasuaji wako wa jicho ukifaulu, Utukufu kwa Mungu," alisema.

Habari hii inakuja baada ya hapo awali Mdee kufunguka kuhusu kuwa kipofu wa jicho moja. 

"Mimi ni kipofu katika jicho moja pia, lakini hiyo haijanizuia kufuata ndoto zangu kubwa."

Baadaye alielezea hali hiyo, akifichua kwamba alikuwa ameishi na tatizo hilo kwa muda

“Nilipata tatizo lililofanya jicho langu kuwa kipofu. Kwa muda nimekuwa nikitumia jicho moja, jingine ni kipofu,” alieleza.

Mdee pia alisisitiza shukrani zake kwa kuona katika jicho lake lililobaki na kushughulikia uvumi unaozunguka hali yake.

Alichapisha vedio akimshukuru Mungu kwa kumtendea wema wa kumponya jicho lake.

Pia aliwashauri watu kuongea na Mungu badala ya kuongea sana kila wakati wanapokuwa kwenye matatizo.

“Wakati mwingine ni bora kukaa kimya tu. na sema na Mungu tu wewe endelea kushughulikia tatizo na sio mtatuzi wa matatizo