Akothee aeleza kwa nini Gen Z wana shauku na kutoogopa

”Dont stigmatise watoto, watoto wanaolelewa na mama peke yake wote wanawajibika kuliko hiyo ndoa unayoitukuza."

Muhtasari

• Aliendelea kumwomba rais kutopitisha mswada wa fedha hadi mazungumzo ya pande zote mbili yatakapofanyika.

• Alisema kuwa kizazi cha Gen Z uende kilipata malezi kutoka kwa  mzazi wa kike peke yake na hii ndiyo sababu hawana woga.

Akothee
Image: Instagram

Gen Z's wameonyesha ujasiri linapokuja suala la kupigania kile wanachoamini kuwa ni sawa.

Wanaendelea kuongoza maandamano ya mswada wa fedha huku wakimwita rais kuja na mswada huo ambao unawathiri wengi.

Mwanamuziki na mfanyibiashara kutoka Kenya Esther Akoth ameandika ujumbe mrefu unaoelezea mapenzi na tabia ya kutoogopa ya Gen Z.

Kupitia Instragram yake, alisimulia uhodari wao wa kulelewa na akina mama wasio na waume.

”Dont stigmatise watoto, watoto wanaolelewa na mama peke yake wote wanawajibika kuliko hiyo ndoa unayoitukuza.

Kizazi Z huenda kililelewa na akina mama wasio na waume kama unavyofikiri na hii ndiyo sababu hawana woga.

Wameshuhudia mama zao wakitupwa nje ya nyumba zao za uzazi, wakiachwa waendelee kuishi au kufa.

Aliendelea kumwomba rais kutopitisha mswada wa fedha hadi mazungumzo ya pande zote mbili yatakapofanyika.

"Hakuna haja ya kucheza ngumu. Ninakuonya—hawana cha kupoteza.

 Wana kila kitu cha kupoteza. Maumivu waliyopitia wa kikua yanatosha kuwatupa mitaani.

 Usiwaguse watoto wa mama pekee. Huenda ikawa kweli kwamba umewalea watoto wako mzazi wa kiume akiwa sasa, lakini ninakusihi uonyeshe ufahamu na huruma.

 Mswada huu wa fedha unapaswa kusitishwa hadi mazungumzo yafanyike” aliandika.

Akothee amekuwa miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamesifu Gen z's kwa ushujaa wao katika kuongoza maandamano.

Maandamano hayo yanatarajiwa kurejelewa kesho.